MANNY PACQUIAO AANZA KUCHEZA LIGI YA KIKAPU YA UFILIPINO
Bondia Manny Pacquiao aliionesha dunia kitu kingine anachoweza nje ya ulingo pale alipovua gloves na kucheza mpira wa kikapu jumapili i...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/manny-pacquiao-aanza-kucheza-ligi-ya.html
Bondia Manny Pacquiao
aliionesha dunia kitu kingine anachoweza nje ya ulingo pale alipovua
gloves na kucheza mpira wa kikapu jumapili iliyopita , ikiwa ni mwezi
mmoja kabla hajapanda ulingoni kutetea mkanda wa WBO.
Pacquiao aliichezea KIA Sorento inayoshiriki lig ya kikapu nchini Philippine.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 alicheza kwa dakika saba, na
kuisaidia timu yake kushinda kwa point 80 dhidi ya 66 dhidi ya
Blackwater Elite kwenye cot ya Philippine Arena.
Pacquiao, amejiunga kwenye timu hiyo kama kocha mchezaji, amecheza
michezo ya kujiandaa na msimu mapema mwezi huu, alifanikiwa kufunga
point moja.
Pamoja na kuwa na urefu wa futi 5 point 6, urefu ambao haufai
kwenye mchezo wa kikapu Pacquiao ni shabiki mkubwa wa mchezo wa mpira
wa kikapu.
Pacquiao atachukua mapumziko kwenye timu yake ya KIA ili kujiwinda
na pambano la uzito wa WBO litakalofanyika November 22 huko Macau dhidi
ya bingwa wa welterweight Chris Algieri.
