Man Utd Kupanda Hadi Nafasi Ya Tatu
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/man-utd-kupanda-hadi-nafasi-ya-tatu.html
Ligi
kuu ya soka nchini Uingereza itaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja
ambapo mabingwa wa kihistoria kwenye ligi hiyo Man Utd watakuwa ugenini
huko The Hawthorns wakipepetana na West Bromwich Albion.
Man
Utd wataingia uwanjani hii leo huku wakijiamini kutokana na mambo
kuwaendelea vyema katika mchezo wao uliopita ambapo waliibanjua Everton
mabao mawili kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.
Kwa
upande wa West Bromwich Albion wao watakuwa wakikumbukia kisago cha
mabao mawili kwa moja walichokipokea kutoka kwa majogoo wa jiji
Liverpool, hivyo hawatokuwa tayari kuangusha point nyingine tatu kwa
mara ya pili mfululizo.
Endapo
Man Utd watafanikisha suala la ushindi hii leo watachupa hadi kwenye
nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
