Kocha na Nigeria, Stephen Keshi na wasaidizi wake watimuliwa
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi amefukuzwa kazi na shirikisho la soka nchini humo, NFF mapema Alhamis hii licha ya ti...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kocha-na-nigeria-stephen-keshi-na.html
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi amefukuzwa kazi na
shirikisho la soka nchini humo, NFF mapema Alhamis hii licha ya timu
yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan jana.
Keshi ametimuliwa pamoja na makocha wake wasaidizi Daniel Amokachi na
Ike Shorunmu. NFF imemshukuru Keshi na wasaidizi wake kwa kazi
waliyoifanya na imeahidi kuwalipa mafao yao ndani ya wiki mbili zijazo.
NFF, imedai kuwa Keshi, Amokachi na Shorounmu wanaweza kuendelea
kusoma course yoyote ya ukocha katika nchi wanayotaka ili kuboresha
uwezo wao.
