KIJANA ALIYEJIUNGA NA IS ATOA ONYO KWA MAREKANI
Baadhi ya watu wanaounga mkono wapiganaji wa IS nchini Iraq na Syria.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/kijana-aliyejiunga-na-is-atoa-onyo-kwa.html
Kijana
raia wa Australia, Abdullah Elmir 'Abu Khaled' aliyejiunga na kundi la
wapiganaji wa IS wanaopigana nchini Iraq na Syria ameonekana kwenye
kanda ya video.
Katika
kanda hiyo kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 anawahutubia waziri mkuu
wa Australia Tony Abbot pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama.
Kundi la wapiganaji wa IS wanaopigana nchini Iraq na Syria.
Kijana huyo alisema "hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi yenu. ''
Alitoroka
kutoka nyumbani Australia mwezi Juni na kijana mwingine raia wa
Australia na inaaminika alisafiri kwenda Syria kupitia Uturuki.
Msemaji wa serikali amesema kanda hiyo ni idhara ya tishop la kundi la Islam ic State kwa dunia nzima.
''Na hiyo ndio maana Australia imejiunga na muungani wa wanjeshi wanaopigana dhidi ya ISIL nchini Iraq,'' alisema msemaji huyo.
Katika
kanda fupi ya video iliyowekwa kwenye mtandao, Abdullah Elmir
waliwahutubia viongozi hao kwa kusema:''Kwa viongozi, kwa Obama,kwa Tony
Abbott nasema hivi, hizi silaha tulizo nazo , wanjeshi hawa hatutakoma
kupigana, hatutasalimisha silaha zetu hadi tutakapofika katika ardhi
yenu. ''
"Hadi
tutakapoweka bendera nyeusi katika kasri ya Buckingham Palace, una hadi
tutakapoweka bendera yetu katika Ikulu ya Marekani, hatutasitisha
vita,'' alisema kijana huyo mwenye umri wa miaka 17.
Source BBC

