INASIKITISHA:- JENERETA LAUA FAMILIA NZIMA NCHINI NIGERIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/inasikitisha-jenereta-laua-familia.html
Mwili
wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke
na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa
gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha
ndani ya nyumba yao .
Katika
dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano
iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia
hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na
kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.
Siku
iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa
kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua
kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na
kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga
walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari,
pikipiki, na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo,
ni sumu inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki
taratibu bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na
kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia
mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani
ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango
imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon
monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama,
ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.

Miili ya watoto watatu wa familia hiyo

