Good Newz! Boko Haram kuwaachilia wanafunzi
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/good-newz-boko-haram-kuwaachilia.html
Serikali
ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa
Boko Haram kuhusu wasichana waliotekwa nyara wa Chibok.
Mkuu
wa jeshi la Nigeria Alex Badeh,aliyefichua makubaliano hayo mwishoni
mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon anasema kuwa
wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo.
Serikali imesema imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi wa Boko Haram.
Kulingana
na afisaa mkuu kiatika ofisi ya Rais Goodluck Jonathan, Hassan Tukur
ambaye alifafanua taarifa hiyo, wajumbe wa serikali walikutana na
wapiganaji wa Boko Haram mara mbili nchini Chad chini ya uongozi wa Rais
wa Chad Idris Derby.
Alisema
kuwa Boko Haram wamekubali kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara
mjini Chibok, hata hivyo, maelezo kuhusu kuachiliwa kwao yatakamilishwa
katika mkutano mwingine utakaofanyika wiki ijayo mjini Njamena.
Pia
alieleza kwamba maafisa wa ujasusi wa Chad walihusika katika mpango huo
na kwamba wamethibitisha mazungumzo hayo yamefikiwa na kukubalika na
kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau.