GHANA YABANWA YATOKA SARE YA 1-1 NA GUINEA KUFUZU AFCON
GHANA imelazimishwa sare ya 1-1 na Guinea katika mechi ya Kundi E kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nc...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/ghana-yabanwa-yatoka-sare-ya-1-1-na.html
GHANA
imelazimishwa sare ya 1-1 na Guinea katika mechi ya Kundi E kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Nahodha
Asamoah Gyan aliwafungia Black Stars kipindi cha kwanza dakika ya 27
kabla ya Ibrahim Traore kuisawazishia Guinea dakika ya 81.
Ghana inabaki kileleni mwa Kundi E kwa
kufikisha pointi tano, wakati Uganda
Bao lililoizamisha Uganda jioni ya jana
lilifungwa
na Donou Kokou dakika ya 30 na matokeo hayo yanaifanya Togo ibebe
pointi tatu za kwanza baada ya awali kupoteza mechi mbili, wakati
Cranes inabaki na pointi zake nne.
Katika
mechi nyingine za jana kufuzu AFCON.ya mwakani Morocco, Gabon iliilaza
2-0 Burkina Faso, mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 67 na 74
mjini Libreville, Sudan iliwafunga mabingwa watetezi, Nigeria 1-0, bao
pekee la Bakri Abd Elgadir dakika ya 41.
Niger
ilitoka sare ya 0-0 na Zambia, Kongo ilifungwa 2-0 nyumbani na Afrika
Kusini, mabao ya Bongani Ndulula dakika ya 52 na Tokelo Anthony Rantie
dakika ya 55, wakati
DRC imefungwa 2-1 nyumbani na Ivory
Coast. Bao la DRC lilifungwa na Cedric
Mongongu dakika ya 71, wakati mabao ya Tembo yalifungwa na Wilfred Bony dakika ya 23 na Max Gradel dakika ya 83.
Msumbiji
iliwafunga 2-0 Cape Verde, mabao ya Saddan Guambe dakika ya 43 na
Artur Faife dakika ya 60, wakati Sierra Leone imetoka sare 0-0 na
Cameroon na Ethiopia ilifungwa 2-0 nyumbani na Mali mabao ya Abdoulay
Diaby dakika ya 33 na Sambou Yatabare dakika ya 60.
Malawi
ilifungwa 2-0 nyumbani na Algeria mabao ya Rafik Halliche dakika ya 10
nabSaphir Taider dakika ya 93. Katika mechi za juzi Senegal ilitoka 0-0
na Tunisia sawa na Lesotho na Angola, wakati Botswana ilifungwa 2-0
nyumbani na Misri mabao ya
Mohamed El Nenny dakika ya 56 na
Mohamed Salah dakika ya 61. Mechi za
marudiano zitachezwa Jumatano zikiwa ni za kwanza katika mzunguko wa pili.
