Balozi Seif Akutana na Muwekezaji kutoka Marekani na Balozi wa Heshima wa Tanzania U S A.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/balozi-seif-akutana-na-muwekezaji.html
Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa
Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake akimtambulisha Makamu wa Rais
wa Kampuni ya maendeleo ya ujkenzi ya Detroit Nchini Marekani Bw. Andrew
G. McLemore kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
walipokutana kwa mazungumzo VIP ya Uwanja wa ndege wa Pemba.Aliyepo kushoto na Balozi Seif ni Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh. Suleiman Saleh.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa
Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya
Ms Shimoja Dr. Robert Shumake kwenye uwanja wa ndege wa Pemba.(Picha na
Hassan Issa OMPR)Na.AOthman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Ms Shimoja kutoka Jimbo la Michigan Nchini Marekani
Dr. Robert Shumake.
Mazungumzo hayo
yamefanyika katika chumba cha watu mashuhuri { VIP } kilichopo kwenye
uwanja wa ndege wa Pemba ambapo Balozi Seif aliwasili akitokea Mjini
Dodoma baada ya kumalizika kwa Bunge Maalum la Katiba.
Katika mazungumzo yao
Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake ambaye
amepata heshima ya kuwa Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani
alielezea kuridhika na mazingira mazuri ya uwekezaji kisiwani Pemba.
Dr. Shumake alisema
Uongozi wa Kampuni yake utaangalia maeneo ambayo inaweza kuwekeza vitega
uchumi kama alivyomuahidi Balozi Seif wakati wa ziara yake katika Jimbo
la Seattle Nchini Marekani mwaka jana.
“
Muda wangu mfupi niliopata kutembelea maeneo tofauti ya Tanzania
ikiwemo Zanzibar umenipa faraja na shauku ya kuangalia fursa zilizopo za
uwekezaji na namna uongozi wa Kampuni yangu utakavyochangamkia fursa
hiyo “. Alisema Dr. Robert Shumake.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo ya Ms. Shimoja kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuupa msaada wakati unaohitaji
kuwekeza hapa Zanzibar.
Balozi
Seif alimueleza Dr. Shumake kwamba Zanzibar tayari imetoa fursa kwa
wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza miradi na vitega uchumi vyao ili
kusaidia kunyanyua pato la taifa sambamba na kuongeza soko la ajira.
Alisema
yapo maeneo na sekta ambazo Kampuni ya Ms Shimoja inaweza kuyatumia
kuwekeza akiyataja kuwa ni patoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa
Pemba, Bandari ya Wete, Sekta ya utalii pamoja na nyumba za mkopo nafuu.
Alifahamisha
kwamba miradi ya nyumba za mikopo nafuu kwa kiasi kikubwa inaweza
kuwasaidia zaidi vijana wenye ajira mpya ili wajenge hatma bora ya
maisha yao ya baadaye.
Dr.
Robert Shumake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms. Shimoja ambae pia ni Balozi
wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani alikuwepo Nchini Tanzania kutia
saini mkataba wa uanzishwaji wa treni iendapo kwa mwendo wa kasi kati
yake na Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania.
Treni
hiyo itakapokamilika itakuwa ikitoa huduma ya usafiri kati ya Dar es
salaamu na pugu kwa kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Kambarage Nyerere.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/10/2014.

