BALOTELLI AAHIDI MABAO LIVERPOOL
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewashukuru mashabiki wa Liverpool kwa sapoti wanayompa na kuwaahidi kucheza vizuri na kufunga mabao....
http://samchardtz.blogspot.com/2014/10/balotelli-aahidi-mabao-liverpool.html
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewashukuru mashabiki wa Liverpool kwa
sapoti wanayompa na kuwaahidi kucheza vizuri na kufunga mabao.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 ameposti kwenye Instagram jana
akishukuru kwa mashabiki wa Anfield kuonyesha imani juu yake na kumpa
heshima kwa kupeperusha bango la kumtukuza.
Bango
hilo liliandikwa kwa lugha ya nyumbani kwao Balotelli, Kitaliano,
likiwa na maana 'Sina cha kuthibitisha zaidi ya ujuzi wangu'.
Na Balotelli amewajibu katika kwa kusema: "Sina cha kuthibitisha zaidi ya ujuzi wangu? Wow asante kwa yeyote aliyefanya hivi.
"Nafahamu
nyote mnatarajia zaidi kutoka kwangu... Mabao zaidi na hususan
ujuzi zaidi, lakini nipeni muda na nitaonyesha ukweli,".
Balotelli amekuwa na mwanzo mgumu
Liverpool, akifunga bao moja tu katika mechi nane alizocheza kwenye mashindano yote
hadi sasa.