TP MAZEMBE YATUPWA NJE KLABU BINGWA AFRIKA ,AS VITA KUCHEZA FAINALI NA SETIF
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/tp-mazembe-yatupwa-nje-klabu-bingwa.html
Entente
Setif ya Algeria imetinga fainali ya Klabu Bingwa Afrika 2014 kwa
magoli ya ugenini, licha ya kupoteza mechi yake 3-2 dhidi ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Kongo.
Mazembe waliopoteza mchezo wa kwanza wa nusu fainali nchini Algeria 2-1, walikuwa wakiongoza kwa 3-1 na kuonekana huenda fainali ingekuwa ya kihistoria dhidi ya AS Vita- kwa mara ya kwanza kati ya timu zote kutoka DRC.
Lakini Setif walipachika bao muhimu la ugenini, dakika 11 kabla ya mpira kumalizika na kujihakikishia nafasi hiyo.
Goli hilo lilifanya matokeo kuwa 4-4, Setif ikiingia fainali kwa sheria
ya magoli ya ugenini na kuifanya klabu hiyo kucheza fainali ya kwanza
tangu waliponyakua Kombe hilo mwaka 1988.
Setif itacheza fainali na AS Vita.
Mchezo wa kwanza wa fainali utachezwa DRC Oktoba 26 na mchezo wa marudiano kuchezwa Algeria Novemba mosi.