PFP KUWATAJIRISHA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI WILAYA 6 NCHINI KUPITIA PROGRAMU YA PANDA MITI KIBIASHARA
Mkurugenzi mtendaji wa PFP Dr Maria Tham akizungumza na wanahabari ofisini kwake Vitalu vya miti vilivyopandwa na wananch...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/pfp-kuwatajirisha-wananchi-wenye-kipato.html
Mkurugenzi mtendaji wa PFP Dr Maria Tham akizungumza na wanahabari ofisini kwake |
Vitalu vya miti vilivyopandwa na wananchi Njombe |
Miche ya miti ambayo mbegu yake imetoka Zimbabwe iliyotolewa na PFP kwa shirika la TANWAT Njombe |
Meneja Mawasiliano wa Mradi, George Matiko wa PFP akiwa katika bustani ya miche ya miti |
Mwanakikundi cha wakulima wa maparachichi Njombe akitunza bustani yake |
Mratibu wa wakulima wadogo wa miti Bw Erasto akizungumza na wanahabari |
Miche ya kisasa ya matunda |
Watenda kazi wa PFP wakimsikiliza mkurugenzi wao |
Mkurugenzi wa PFP akiendelea kutoa ufafanuzi wa mradi |
Afisa habari wa PFP Bi Lilian akichukua taarifa juu ni wafanyakazi wenzake |
Wanakikundi cha miti Kifanya wakiwajibika kujitafutia utajiri kwa kupanda miti |
Wanakikundi cha upandaji miti kibiashara Kifanya wakiwa katika kitalu chao
Moja ya kitalu cha kuotesha miche ya miti kilichopo katika kijiji cha Kifanya wilayani Njombe; kitalu hicho ni cha wakulima wanaounda umoja wa wapanda miti Kifanya |
Meneja Mawasiliano wa Mradi, George Matiko akifafanua jambo kwa wanahabari; aliyeketi ni Mkurugenzi wa Programu hiyo, Dk Maria Tham |
Dk Maria Tham katika mahojiano na wanahabari ndani ya ofisi zao zilizopo mjini Njombe |
Mwenyekiti wa kikundi cha wapanda miti wa kijiji cha Kifanya akitoa ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na kikundi chao |
Na Matukiodaima.co.tz Njombe
WANYANCHI
wenye kipato katika wilaya 6 za mkoa wa Njombe ,Iringa na Morogoro
wanatarajia kunufaika kiuchumi kupitia programu maalum ya Panda Miti
Kibiashara(PFP) ambayo imeanza na mpango huo kwa kasi kubwa .
PFP
imeanzisha programu hiyo ili kuwaondoa katika hali ya umasikini na
kuwawezesha kupata maisha bora zaidi kwa kuanzisha kilimo hicho
cha miti badala ya ilivyosasa kwa wakulima wengi kutegemea mazao
ya biashara pekee na pale soko linaposhindikana hali ya maisha
kiuchumi huyumba zaidi.
Akizungumza
na wanahabari ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa PFP Dk Maria Tham
alisema kuwa wilaya zitakazonufaika na mradi huo ni ,Kilolo na Mufindi
kwa mkoa wa Iringa na mkoa wa Njombe ni Ludewa , Makete, Njombe wakati
mkoa wa Morogoro ni wilaya moja pekee ya Kilombelo .
Alisema
biashara ya miti itaongezeka kwa kuzingatia kwamba ifikapo mwaka 2025
inatarajiwa mahitaji ya malighafi viwandani na kuni yataongezeka kutoka
mita za ujazo milioni 1.5 hadi milioni 3.7.
Hata
hivyo Dk Tham alisema lengo kuu la program hiyo iliyoanza Januari
mwaka huu ni kuongeza kipato kwa wananchi vijijini kwa kuwapa elimu
ya upandaji wa miti kitaalamu kwa kutumia mbegu bora na kuhudumia
mashamba ipasavyo kwa kuzingatia mipango ya matumizi endelevu ya ardhi.
“ Wananchi wanapanda miti ila bado hawapandi kitaalam na wengi wao wanavuna miti michanga zaidi na hivyo kukosa faida "
Alisema
kuwa lengo kuu la program ni kuona wananchi wanapanda miti kisasa
hasa ukizingatia kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina udongo
unaofaa kukuza miti, mvua za kutosha, ardhi ya kutosha na wakazi wake
wanapenda kupanda miti japo utaalam bado .
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa kwa kupitia program hiyo mipango ya matumizi
endelevu ya ardhi itatengenezwa huku wananchi wanaopanda miti
wakihamasishwa kuunda vikundi vya wakulima wa miti kwa nia ya
kufanikisha shughuli za upandaji miti.
Katika
kipindi cha miaka minne kuanzia sasa wananchi katika wilaya hizo
watahamasishwa kupanda miti katika eneo lenye ukubwa wa hekta 15,000.
“Huku
wakihimizwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato wakati
wakisubiri miti yao ikue na kufikia umri unaofaa kuvunwa,” alisema.
mratibu
wa mtandao wa wakulima wapandaji miti ya matunda Njombe na Mufindi
Erasto Ngole alisema kuwa toka PFP wamefika katika wilaya zao hali
ya wakulima kujiunga na vikundi vya upandaji miti ya matunda na ile ya
mbao na nguzo uimeongezeka zaidi .