MOURINHO AFUNGUA TENA VITA YA MANENO NA MANUEL PELLEGRINI, ADAI 'ALIMUUA' CLATTENBURG
+10 Kocha wa Chelsea , Jose Mourinho amedai kuwa Manuel Pellegrini 'alimuua' Mark Clattenburg mapema msimu...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/09/mourinho-afungua-tena-vita-ya-maneno-na.html
Kocha wa Chelsea , Jose Mourinho amedai kuwa Manuel Pellegrini 'alimuua' Mark Clattenburg mapema msimu huu.
JOSE Mourinho amemjia juu kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini akidai 'alimuua' mwamuzi Mark Clattenburg’.
Pellegrini alimkosoa kocha huyo wa
Chelsea baada ya sare ya 1-1 baina ya timu hizo uwanja wa Etihad
jumapili iliyopita na alimshutumu Mourinho kuwa alicheza mechi hiyo kama
'timu ndogo'.
Hatimaye Mourinho alijibu mapigo jana
akimkumbusha Pellegrini ambaye ni mara chache sana kujihusisha kwenye
migogoro kuwa alivunja kanuni zake mwenyewe za msimu uliopita kwa
kumkosoa Clattenburg.
Frank Lampard aligoma kushangilia baada ya kuifungia Man City bao la kusawazisha dhidi ya Chelsea
Mwamuzi Clattenburg alimuonesha kadi ya njano, Lampard katika sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal mapema mwezi huu
Kocha wa Man City , Pellegrini alidai uchezeshaji mbaya wa Clattenburg ulimkosesha ushindi katika uwanja wa Emirates
Mourinho alisema: "Sio mara moja, mbili au tatu alimuambia kila mtu kuwa hazungumzi kuhusu waamuzi. Alimuua Clattenburg".
"Mara tatu au nne alisema hazungumzi
kuhusu mimi au timu yangu-amefanya tena. Ni juu yako kutoa maoni.
Niliposema sitaki kumzungumzia yeye, ndicho najaribu kufanya".