YALE MAGARI YASIYOKUWA NA DEREVA RASMI KUTEMBEA NCHINI UINGEREZA_2015
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/yale-magari-yasiyokuwa-na-dereva-rasmi.html

Gari linalojiendesha
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.
Serikali hiyo pia imetoa wito miji ya Uingereza
zitoe mapendekezo ya kuwania kuwa wenyeji wa moja kati ya majaribio 3
ya magari hayo.Aidha waziri huyo ameagiza kufanywe mabadiliko ya sheria za barabarani ilikuafikiana na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Wizara ya usafiri wa umma nchini Uingereza ilikuwa imeahidi kuruhusu majaribio ya magari hayo mwisho wa mwaka uliopita.
Katibu wa Biashara Vince Cable aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Mira,kilichoko Midlands.
"tangazo hili la leo linatoa ithibati kuwa magari pasi na madereva yatakuwa barabarani katika miezi 6 zijazo''.

Uingereza kuruhusu magari bila ya dereva katika miezi 6 ijayo
Wadau hata hivyo wamekuwa wakiibua tahadhari ya maswala ya Bima,na uhalali wa magari pasi na madereva jambo ambalo limewalazimu kutumia barabra za kibinafsi kwa majaribio yao.
''Mimi mwenyewe nilijiskia kuwa salama ndani ya gari hilo lililokuwa bila dereva''alisema bwana Cable.
Wakati huohuo Magari hayo yameruhusiwa kufanyiwa majaribio huko Marekani katika majimbo ya California, Nevada na Florida.

Nissan imeruhusiwa kujaribu magari bila ya dereva
Mwaka uliopita kampuni ya 2013 ilifanya majaribio ya gari lake huko Japan.
Barani Uropa kampuni ya kutengeza magari ya Volvo tayari imepata ithibati ya kujaribu magari yake mjini
Gothenburg Sweden.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu