U.S.A YASHAMBILIA WANAMGAMBO WA IS
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/usa-yashambilia-wanamgambo-wa-is.html
Ndege za Marekani zilizotekeleza mashambulizi dhidi ya IS
Wizara ya
ulinzi nchini Marekani inasema kuwa ndege za jeshi la Marekani
zimefanya mashambulizi ya angani dhidi wanamgambo wa kundi la Islamic
state kaskazini mwa Iraq.Pentagon
ilisema kuwa ndege zilishambulia vituo vilivyokuwa vikitumiwa
kushambulia vikosi vya kikurdi vinavyopigana kulinda ngome ya mji wa mji
wa Irbil.Siku
ya Alhamisi rais wa marekani Barack Obama aliamrisha kufanyika kwa
mashambulizi ya angani dhidi ya wanamgambo wa kisuni ambao wameteka
kiasi kikubwa cha ardhi ndani ya Iraq na pia ndani ya Syria.

Jamii ya Yazidi inayolengwa na IS
Rais
Obama alisema kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State watalengwa iwapo
wataelekea kwenye mji wa kikurdi wa Irbil au kwa lengo la kuzuia kile
alichokitaja kama vitendo vya mauaji ya halaiki dhidi ya wakristo na
jamii za Yazidi.
Hatua ya
Marekani inajiri kukiwa na wasiwasi mkubwa wa uwezo wa wanamgambo hao
kuteka sehemu kubwa zaidi ya Kaskazini mwa Iraq mbali na sehemu kubwa ya
Syria.
Rais
Obama amewashutmu wanamgambo wa Islamic State kwa kujaribu kuiangamiza
jamii nzima na ya Yazidi akisema kuwa serikali yake itachukua hatua za
kuzuia kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Wapiganaji wa Kikurdi wanaokabiliana na IS
Ndege za
jeshi la marekani zimekuwa zikiangusha misaada huku nayo Uingereza
ikisema kuwa itajiunga kwenye jitihada za kutoa misada.
Kiongozi
wa dhebu la shia nchini Iraq Ayatollah Ali al Sistani amewataka
wanasiasa nchini Iraq kungana na kumaliza ghasia huku naye kiongozi wa
kanisa katoliki duniani papa Francis akisema kuwa atatuma mmoja wa
viongozi wa kanisa hilo kama njia ya kuonyesha umoja .
Mnamo
mwezi juni IS, awali ikijulikana kama Isis, iliteka mji wa Mosul kisha
kundi hilo likauteka mji wa wenye wakristu wengi Qaraqosh.

Wakimbizi wa ndani kwa ndani Iraq
Kulingana
na Idara ya usalama ya Marekani Pentagon ndege mbili za F/A-18
zilidondosha mabomu yenye paundi 500 ilikukaharibu ngome ya mashambulizi
ya IS inayotumika kuishambulia mji wa Irbil.
Mji huo wa Irbil ni mwenyeji wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani.
Hii ndiyo mara ya kwanza kwa jeshi la Marekani kujihusisha katika mapigano ndani ya Iraq tangu mwaka wa 2011.
Waziri wa
maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry ameonya jamii ya kimataifa
kugutuka na kutahadhari dhidi ya ufanisi wa kundi hilo la wanamgambo wa
IS.
CREDIT:BBC
