TETESI ZA SOKA KATIKA MAGAZETI YA BARANI ULAYA..! HIZI HAPA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/tetesi-za-soka-katika-magazeti-ya.html
Atlètico Madrid wapo tayari kutoa pauni
milioni 25 kuwasajili Javier Hernandez, 26 na Shinji Kagawa, 25, kutoka
Manchester United (Guardian), Barcelona wana wasiwasi wa kushindwa mbio
za kumsajili Juan Cuadrado, 26, ambaye
anasakwa na Manchester United kwa pauni milioni 29 (Daily Star),
Liverpool na Tottenham wapo tayari kumfuatilia mshambuliaji kutoka Ivory
Coast Wilfried Bony, 25, wakati Swansea wakifikiria kuondoa kifungu cha
utenguzi cha pauni milioni 19 cha uhamisho (Daily Mirror), beki wa
Arsenal Thomas Vermaelen hatojadili mkataba mpya na Arsenal, katika
jitihada zake za kulazimisha uhamisho kwenda Barcelona au Manchester
United (Sun), Everton bado wanafikiria kuongeza wachezaji, na
wanamfuatilia kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 24 (Daily Mail),
Tottenham wanakaribia kukamilisha kumsajili beki wa kati kutoka
Argentina, Mateo Musacchio, 23, kutoka Villareal na wapo tayari kumuuza
Younes Kaboul, 28, ambaye huenda akahamia Lazio kwa pauni milioni 6
(Telegraph), Pepe Reina huenda akabakia Liverpool baada ya AC Milan
kushindwa na mshahara anaotaka (Independent), Sunderland wapo tayari
kumfuatilia Samuel Eto'o ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka
Chelsea (Talksport), matumaini ya Liverpool na Manchester Unitedyamezizima baada ya kiungo Marco Reus kusisitiza kuwa atabakia Borussia
Dortmund msimu ujao (Metro), Louis van Gaal ataamua wiki hii, nani
anabaki na nani anaondoka wakati atakapokamilisha mipango yake ya
usajili na Ed Woodward. Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane
Fellaini huenda wakauzwa (Daily Telegraph), Liverpool wanapanda dau la
pauni milioni 5 kumtaka beki wa Barcelona Dani Alves, 31
(Mundodeportivo), Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 23.9 kumsajili
kiungo wa Sporting Lisbon William Carvahlo (O Jogo), beki wa kulia wa
Atlètico Madrid Javier Manquillo amewasili Uingereza kufanya vipimo vya
afya kabla ya kujiunga na Liverpool (Daily Mail). Tetesi Na salim kikeke nyingine kesho
tukijaaliwa- nawatakia siku njema, Cheers!!!