Obama awataka viongozi Iraq waungane
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/obama-awataka-viongozi-iraq-waungane.html
Rais wa Marekani Barack Obama
ameonya kuwa hakuna njia rahisi ya kuisaidia serikali dhaifu ya Iraq
kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State.
''Itachukua muda mrefu kwa majeshi yetu kuisidia
Iraq kuwashinda wapiganaji wa Kisunni ambao wametangaza himaya yao
inayojumuisha ardhi katika mataifa ya Iraq na Syria ''Alisema Obama.
Majeshi ya Marekani yashambulia Wapiganaji Islamic State
Rais Obama aliruhusu majeshi yake kuishambulia ngome ya Islamic State Ijumaa kwa mara ya kwanza ambapo majeshi ya Marekani imehusika katika vita moja kwa moja nchini Iraq tangu mwaka wa 2011.

Wakimbizi kutoka jamii ya Yazidi wakitorokea maisha yao
Mapema leo ndege za kijeshi za Uingereza zimefunga safari kusaidia utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Iraq.
