MSF:Kambi ya Bentiu Sudan Kusini haifai
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/msfkambi-ya-bentiu-sudan-kusini-haifai.html
Shirika la madaktari wasio na
mipaka MSF limesema kuwa takriban watu elfu arubaini wanaishi katika
mazingira mabaya katika kambi moja ya umoja wa mataifa nchini Sudan
Kusini.
Shirika hilo limesema kuwa maelfu ya raia
wanaishi katika eneo lenye mafuriko yaliochanganyika na maji taka katika
kambi ya Bentiu ambapo wamekimbilia hifadhi ili kukwepa vita kati ya
vikosi vya serikali na waasi wa taifa hilo.Limesema kuwa raia wengi katika kambi hiyo hawawezi kulala na hivyobasi husalia kusimama wakiwabeba wana wao.
MSF limesema kuwa mazingira hayo ni ukiukwaji wa utu wa kibinaadamu.
