MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE AZINDUA MAKTABA YA KISASA SHULE YA SEKONDARI CHALINZE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mbunge-wa-jimbo-la-chalinze-azindua.html
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya
shule ya sekondari ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo imejengwa na
Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa
kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya shilingi
milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo, Mbunge
huyo pia ameahidi kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta
ili wanafunzi wajengewe mzingira mazuri zaidi ya kujisomea lakini pia
ameahidi kushughulikia tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru kwenda
kidato cha ano na sita lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa, hivyo
ameueleza uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi kwamba wanafunzi hao
lazima watafutiwe nafasi ya kuendelea na shule hata kama itakuwa siyo
ndani ya jimbo la Chalinze, "Muhimu wapate nafasi ya kuendelea na elimu
yao ya kidato cha tano na sita" Alisema Mh. Ridhiwani Kikwete alimuomba
mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw. Mbwana Madeni amkabidhi majina ya
wanafunzi wote kumi ili yaanze kufanyiwa kazi mara moja.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti
wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya
kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka
taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi
ya Read International pia.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali
vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma
kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za
kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati akikagua
maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake kama
kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya
sekondari ya Chalinze.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa
bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma
risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoa
taasisi ya Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya
sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba
katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya
shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo
la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari
Dk Fadhil Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana
jijini dar es salaam.
Meneja masoko
wa Simba Cement Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati
wa uzinduzi wa Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo
gharama yake ikiwa ni shilingi milioni 42 za kitanzania. PICHA NA
FULLSHANGWE BLOG








