Flatnews

Mazoezi Yanga sasa ni kimya kimya!


Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo 
By LASTECK ALFRED  (email the author)
  • Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo amesema kuwa waandishi na watu wengine wachache wataruhusiwa kuangalia kidogo na kuzungumza naye siku ya Ijumaa tu. Bosi huyo amesisitiza kuwa anafanya hivyo ili kuficha siri zake na watu wasione mbinu zake kwani mambo yanavuja sana na hata wapinzani wao wanawasoma sana kiufundi.

YANGA itakwenda Zanzibar keshokutwa Jumatatu kuweka kambi ya siku 10, lakini ikirejea Dar es Salaam kila kitu mazoezini kitakuwa siri na hakuna yeyote atakayeruhusiwa kushuhudia kama si mchezaji. Itakuwa hivyo hata kwa viongozi.
Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo amesema kuwa waandishi na watu wengine wachache wataruhusiwa kuangalia kidogo na kuzungumza naye siku ya Ijumaa tu. Bosi huyo amesisitiza kuwa anafanya hivyo ili kuficha siri zake na watu wasione mbinu zake kwani mambo yanavuja sana na hata wapinzani wao wanawasoma sana kiufundi.
Kambi hiyo ya visiwani Pemba ni sehemu tu ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara na mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam FC.
 “Ninapenda kuwaomba radhi waandishi wa habari pamoja na wapenzi wa Yanga ambao wamekuwa wakifuatilia mazoezi kila mara kwa kuwa hawataweza kuona kinachoendelea mazoezini kwa takribani wiki tatu tukitoka Pemba,” alisema.
“Kuna vitu ni siri na kuna mbinu na mafunzo maalumu ambayo nitawapa wachezaji wangu ambavyo havitakiwi kuonekana na mtu yeyote nje ya kikosi.
“Lengo langu ni kuwa na timu pamoja kwa karibu na kuwapa ujuzi wa ziada ambao utakuwa na manufaa kwa timu na itakuwa siri ya mafanikio yetu.”
Mara kadhaa makocha mbalimbali wamekuwa wakitiririka kuangalia mazoezi anayotoa Maximo kwa wachezaji wake kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari wa Loyola jijini Dar es Salaam baadhi ya makocha kama Mbwana Makatta, Shija Renatus waliwahi kuhudhuria na kuona mbinu hizo.
Maximo alisema: “Nahitaji usiri ili vitu ambavyo nitafundisha viwe na manufaa. Nataka kufanya kama Ufaransa na Ujerumani wakati wa Kombe la Dunia, hawa walikuwa hawaonyeshi mbinu zao, nikienda na mfumo huo ndiyo nitaweza kufika mbali, Brazil ilikwama kwa sababu ya kuonesha mbinu mbalimbali ambazo baadaye wapinzani wao walizisoma.”
Yanga imepanga kucheza mechi mbili za kirafiki wakati itakapokuwa Pemba ili kuanza kuwapa wachezaji wake uzoefu wa mechi za ushindani na pia kumsaidia Maximo kupata kikosi cha kwanza.
Maximo aliongeza: “Jaja anajitahidi siku hadi siku, nina furaha kuwa mambo yanaenda vizuri. Tatizo kubwa ni kuwa yeye na Coutinho (Andrey) walikuja Tanzania wakiwa hawapo kwenye viwango vyao baada ya kuwa nje ya uwanja kwa ajili ya mapumziko kwani ligi ya Brazil ilikuwa imekwisha.”
Awapa mbinu mastraika
Maximo anaonekana kuamini kombinesheni ya mastaika Jerry Tegete na Jaja na kwa hilo amewapa mbinu za jinsi ya kuwachanganya mabeki wa timu pinzani.

Post a Comment

emo-but-icon

item