MAPACHA WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA MKOANI GEITA WAFARIKI DUNIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/mapacha-waliozaliwa-wakiwa-wameungana.html
Watoto
wawili mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana tumbo na kifua, wamefariki
muda mchache baada ya kuzaliwa katika kituo cha afya Katoro wilaya ya
Geita mkoani Geita. Akizungumza,
mama wa watoto hao, Neema Luswetura (23), alisema alijifunga Agosti 6,
muda mchache baada ya kufikishwa katika kituo hicho cha afya.
Muuguzi wa zamu katika kituo hicho, Joyce
Michael akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema walimpokea
mwanamke huyo saa 7 usiku akilalamika uchungu, na hivyo kupelekwa wodi
ya wazazi na asubuhi alijifungua watoto wenye uzito wa kilo 5.1 wakiwa
wameshikana na kufariki.
Alisema wakati wa zoezi la kumzalisha,
alilazimika kuomba msaada toka kwa mganga wa zamu, Dk. Daniel Izengo
ili kunusuru uhai wa mama huyo lakini watoto wake hawakuweza kupona.
Dk. Izengo alithibitisha kuwepo kwa tukio
hilo na juhudi za kunusuru uhai wa watoto hao zilishindikana, akieleza
kitalaam tukio hilo linajulikana (coujoined twins).
Kutokana na hali hiyo, Dk. Izengo ameishauru jamii hususani wajawazito kuzingatia ushauri wanaopewa na madaktari.