KLABU VPL, FDL ZATAKIWA KUWASILISHA MABENCHI YA UFUNDI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/klabu-vpl-fdl-zatakiwa-kuwasilisha.html
Klabu
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinatakiwa
kuwasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) orodha ya
watendaji wa mabenchi yao ya ufundi yakiongozwa na Kocha Mkuu.
Ni wajibu wa klabu kuhakikisha zinatekeleza maagizo hayo kwani ni matakwa ya Kanuni za VPL na zile za FDL.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itaanza kutimua
vumbi Septemba 20 mwaka huu wakati ile ya FDL inatarajia kuanza Oktoba
mwaka huu.
