Jack Rodwell akimbia Man City na kujiunga Sunderland
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/jack-rodwell-akimbia-man-city-na.html
Sunderland
imemsajili kiungo wa Manchester City Jack Rodwell kwa mkataba wa miaka
miatno ikiwa ni sehemu ya kukiimarisha kikosi hicho kwa ajili msimu ujao
wa ligi.
Kinda huyo wa kimataifa wa England, 23, amejiunga na klabu hiyo kwa ada ya paundi 10m.
"Soka la uhakika ni kitu muhimu sana kwangu," Rodwell aliiambia website ya Sunderland. "Hii ni sehemu kubwa kwangu." Rodwell alijiunga
na City akitokea Everton kwa ada ya paundi 12m mwaka 2012 lakini
amecheza mara 26 tu na kufunga mabao mawili kutokana na kukumbwa na
majeruhi ya mara kwa mara jambo ambalo lilitoa nafasi kwa viungo wengine
kufanya kazi.
JACK RODWELL |
|---|
| Aliichezea Everton kwa mara ya kwanza dhidi ya AZ Alkmaar December 2007, akiwa na umri wa miaka 16 na siku 284 - na kuwa mchezaji mdogo zaidi kuiwakilisha Everton Europe |
| Alicheza michezo 85 akiwa na the Toffees, na kufunga mara nne |
| Alijiunga na Manchester City kwa uhamisho wa paundi 12m na kusaini mkataba wa miaka mitano August 2012 |
| Alicheza micheo 16 na kufunga mara mbili akiwa na City |
| Aliichezea England kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Uhispania ambapo walishinda 1-0 November 2011 na akaichezea katika michezo dhidi ya Sweden na Brazil |
