Hii ndio klabu kubwa nchini Uingereza ambayo Rihanna ameripotiwa kutaka kuinunua
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/hii-ndio-klabu-kubwa-nchini-uingereza.html
Moja ya watu maarufu waliokumbwa na joto kubwa la soka wakati wa michuano ya kombe la dunia, alikuwa ni mwanamuziki Rihanna.
Alikuwa akituma tweets karibia kwenye michezo yote na mwishoni
alienda kuhudhuria fainali ya michuano hiyo iliyopigwa kwenye dimba la
Maracana kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina.
Siku kadhaa nyuma gazeti la Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba
staa huyo alikuwa anajiandaa kununua hisa kwenye moja ya vilabu vikubwa
nchini Uingereza, lakini hawakutaja jina la timu.
Lakini leo hii Jumanne, gazeti moja huko Catalunya liitwalo El Mundo
Deportivo limethibitisha kwamba Rihanna anataka kununua hisa nyingi
kwenye klabu ya Liverpool.
Rihanna amewahi kuripotiwa kwamba anaishabikia klabu ya Liverpool,
jambo ambalo inawezekana El Mundo Deportivo wamemhusisha na ununuzi wa
klabu hiyo ya Anfield.
Liverpool kwa sasa inamilikiwa na mmiliki wa makampuni ya American Fenway Sports Group John W. Henry.