GLASGOW: VIONGOZI WA RT WANAYO AGENDA YAO YA SIRI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/glasgow-viongozi-wa-rt-wanayo-agenda.html

December mwaka jana Andrea
Sambu naMusanduki Mohamed walifikia viwango ‘TAKATIFU’ vya ushiriki wa
Commonwealth Games ila kwa sababu ya “Agenda yao ya
Siri” hawakujumuishwa timu ya Glasgow.
Hivyo kwa ubabe kabisa RT walikataa bila maelezo ni kwa nini waliwaacha wanariadha hao.
Hivyo Tanzania tumekosa medali kwa sababu zifuatazo;
- Waliamua kumwacha
Andrea Sambu kwa sababu aliyemuandalia mbio za China ni Wilhelm
Gidabuday ambaye RT wanaona ni adui wao mkubwa sababu ya kuwa mkweli
- Je watanzania wakose
MEDALI kwa sababu ya ubabe wa viongozi wa RT na hatimaye Tanzania kukosa
sifa wakati FEDHA ZA WALIPA KODI zimetumika ili taifa liondokane na
aibu.
- Ifahamike wazi bila
kupepesa kwamba RT inaongozwa na viongozi FEKI sababu hawakuchaguliwa
kwa katiba ya RT wala kwa SHERIA # 12 ya BMT iliyotungwa na BUNGE 1967.
- ANDREA SAMBU SIPE
Fedha alizotoa Waziri Membe
hazikuingizwa account ya RT; Je Mheshimiwa Membe aliweka fedha hizo
kwenye box akawakabidhi rundo la minoti? TUNGEPENDA MEMBE AFAFANUE!
- Vinginevyo nia yake
njema inaweza kutafsiriwa vinginevyo maana hivi sasa siasa imeshaingilia
viwanja vya michezo ndiyo maana DC Mtaka anatafuta CV kupitia Chama Cha
Riadha (RT).
- Je timu ya riadha ya
kwenda kambi za nje ilichaguliwa kwa VIGEZO GANI? Bilashaka Waziri Membe
angelihakikisha kwamba fedha anazozitoa zinakwenda kufanya ‘Intended
Mission’.
- Pia Waziri Membe
afahamu kwamba kuna watu watatu ambao
walifanikisha‘Proposal’ aliyoletewa ambayo ilikuwa na neno “SPORTS
DIPLOMACY” watu hao ni Mwalimu Samwel Tupa, Wilhelm Gidabuday na Thabit
Bashir.
- Inashangaza sana
kwamba William Kallaghe anaficha ukweli wa ushiriki wa wadau wa riadha
waliotumia muda wao mkubwa kuandaa mchanganuo ambao ndiyo sasa
unajulikana kwa jina zuri sana la “SPORTS DIPLOMACY”
“WANARIADHA WOTE KWA SAUTI MOJA
TUNAMTAKA WAZIRI MEMBE AWASHIRIKISHE WADAU MUHIMU SIKU RIPOTI YA GLASGOW
INAPOWASILISHWA ILI KILA ALIYE MTAALAM WA MICHEZO APATE KUTOA WAZO LAKE
KWA NIA NJEMA YA KUBORESHA TIMU YETU SIKU ZA USONI
Chanzo: shaffihdauda.com
