BALOZI WA UJERUMANI NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE D’SALAAM
http://samchardtz.blogspot.com/2014/08/balozi-wa-ujerumani-nchini-amtembelea.html
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza
Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke alipokuwa akimfafanulia jambo
wakati Balozi huyo na Naibu wake walipomtembelea Waziri huyo ofisini
kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali
ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimfafanulia
jambo Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke wakati Balozi huyo na
Naibu wake, John Reyels (kulia) walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini
kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali
ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiagana na Naibu
Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels wakati Naibu huyo na Balozi
wake, Egon Kochanke (katikati) walipomaliza mazungumzo na Waziri Chikawe
ofisini kwake Dar es Salaam baada ya kujadiliana masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Ubalozi huo na Wizara yake. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.