WITO WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAX ADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wito-wadau-kutoa-maoni-ya-miswada-ya.html
BUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
WADAU KUTOA MAONI YA MISWADA YA SHERIA YA: VALUE ADDED TAX ACT, 2014, TAXADMINISTRATION ACT, 2014 NA FINANCE ACT, 2014
_____________
Katibu
wa Bunge anawatangazia wananchi wote kwamba Kamati ya Bunge ya Bajeti
itaanza kuchambua Miswada ya Sheria ya: Value Added Tax Act, 2014, Tax
Administration Act, 2014 na Finance Act, 2014 siku ya Jumanne tarehe 17
Juni, 2014 kwa lengo la kuuboresha kabla ya kupelekwa Bungeni kusomwa
mara ya pili na hatimaye kutungwa kuwa Sheria.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 84(2) ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la April,
2013 Kamati ya Bunge iliyopelekewa Muswada na Mheshimiwa Spika inaweza
kumwalika mtu yeyote au taasisi yoyote kwa njia ya matangazo au kwa
kuwaandikia barua ya mwaliko kufika mbele ya Kamati na kutoa maoni yao.Hivyo
basi, Kamati ya Bajeti inakaribisha wadau wenye maoni ya kuboresha
miswada ya Value Added Tax Act, 2014, Tax Administration Act, 2014
kuwasilisha maoni hayo kwa Maandishi kwa Katibu wa Bunge, Ofisi ya
Bunge, S.L.P 941, Dodoma. Kikao cha kusikiliza na kupokea maoni hayo
kitafanyika siku ya Jumanne tarehe 17 na Jumatano tarehe 18 Juni, 2014.
Maoni
kwa ajili ya Finance Act yatapokelewa na kusikilizwa siku ya Alhamisi
tarehe 19 na Ijumaa tarehe 20 Juni, 2014. Aidha, Kamati inapendekeza
kuwa maoni yawasilishwe kupitia makundi ama asasi zenye maslahi
yanayofanana ili yaweze kushughulikiwa kwa pamoja.
Maoni
kuhusu Miswada hiyo, yatasikilizwa katika tarehe tajwa kuanzia saa 5.00
asubuhi, Ukumbi wa Msekwa uliopo Bungeni Dodoma. Aidha, maoni hayo
yanaweza kutumwa kwa njia ya barua pepe kwa anuani lkitosi@parliament.go.tz. Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na Sekretarieti ya Kamati kupitia nambari +255716909526, +255785570685 au +255756160006.
Miswada hiyo inapatikana katika Tovuti ya Bunge www.parliament.go.tz.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DODOMA
14 Juni 2014
