Flatnews

Wapiganaji wavamia kituo cha mafuta Iraq


Wapiganaji wa madhehebu ya Sunni
Wapiganaji wa madhehebu ya Sunni wamekishambulia kiwanda kikubwa mno cha kusafisha mafuta katika mji wa Baiji, Kaskazini mwa Iraq kwa kutumia mizinga na makombora.
Duru zasema kuwa walinzi watano wa Iraq wameuawa katika shambulio hilo.
Kuna habari kuwa Majeshi ya Iraq pia yalituma ndege yake ya Helikopta, ambayo kwa bahati mbaya imelipua tenki moja kubwa ya kuhifadhia mafuta kwa kombora na Kusababisha moto mkubwa.
Shughuli zilisitishwa siku chache zilizopita za uzalishaji wa mafuta kutoka katika kituo hicho na wafanyakazi wa kigeni wakamarishwa kuondoka.
Makabiliano pia yameshuhudiwa katika mji wa Ramadi Mashariki mwa nchi hiyo.
Kituo cha kusafishia mafuta kilicho shambuliwa
Serikali inakabiliana na wapiganaji wa ISIS na washirika wake wa Sunni Muslim katika miji ya Diyala na Salahuddin baada ya wapiganaji kuvamia mji wa pili Mosula kwa mara ya kwanza wiki jana.
Waziri mkuu Nouri al-Maliki, alionekana kupitia televisheni na viongozi wa Sunni na wakurdi Jumanne ili kutoa wito wa amani na umoja huku wapiganaji wakijiandaa kwa vita zaidi.
Wanataka watu wanaomiliki silaha na ambao sio wanajeshi wa serikali kusalimisha silaha hizo.
Wapiganaji wa Sunni walliojitolea kupigana
Hata hivyo wito huo huenda usilete mabadiliko makubwa huku bwana Maliki akitoa wito wa wanajeshi wa kishia kushirikiana na wanajeshi wa Iraq kupambana dhidi ya wapiganaji hao.
Mamia ya watu wameuawa tangu mapigazo kuzuka nchini humo wiki jana , wengi wakiaminika kuwa wanajeshi waliotekwa nyara na kupigwa risasi na wapiganaji wa ISIS.
Wakati makabiliano yalipokuwa yanaendelea mjini Baquba, wafungwa 44 waliuawa ndani ya kituo cha polisi katika hali ya kutatanisha

Post a Comment

emo-but-icon

item