Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakutana Brussels
Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujaribu kuupatia ufumbuzi mvutano uliosababishwa na Uingereza kuhusu kuteuli...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/viongozi-wa-umoja-wa-ulaya-wakutana.html
Viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kujaribu
kuupatia ufumbuzi mvutano uliosababishwa na Uingereza kuhusu kuteuliwa
Jean-Claude Juncker kuwa mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani (kulia) akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron."Si haki kwamba viongozi waliochaguliwa wa serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya waachilie mbali haki yao ya kumteuwa kiongozi wa halmashauri kuu. Ni muongozo mbaya na anayechaguliwa pia hafai. Jean-Claude Juncker ni mshika bendera wa mradi wa kuuzidishia madaraka Umoja wa Ulaya na kuyapunguzia madaraka mataifa wanachama. Yeye si mtu anaefaa kuiongoza halmashauri hii." Anasema Cameron
Majadiliano moto moto yanategemewa
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron (kushoto), na Jean Claude
Juncker anayetarajiwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya
Umoja wa Ulaya.Viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya, tangu wa mrego wa kihafidhina mpaka wa mrengo wa shoto, wanamuunga mkono Juncker. Walipofika katika ukumbi wa mkutano, hakuna yeyote aliyesema chochote kuhusu hilo - si Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na wala Rais Francois Hollande wa Ufaransa.
Wito wa mageuzi unapingwa na wahafidhina
Viongozi wa vyama vya Social Democratic barani Ulaya wamuunga mkono
Jean Claude Juncker kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa
Ulaya.Naye Waziri Mkuu wa Ubelgiji, Elio Di Ripo, licha ya kukiri kwamba msimamo wa Uingereza unaeleweka na unastahiki sifa, lakini ameonya kwamba taifa hilo haliwezi peke yake "kuwazuwia wenzao 26 ambao wanamtaka Juncker."
Viongozi wa Social Democratic wakiongozwa na Rais Hollande wameelezea uungaji mkono wao kwa Juncker tangu mwishoni mwa wiki iliyopita. Hata hivyo, wanataka badala yake watu waregeze kamba katika baadhi ya masuala kama vile bajeti ili kuunga mkono uwekezaji na ukuaji wa kiuchumi. Lakini madai hayo yanakataliwa na wahafidhina wakiongozwa na Kansela Merkel.