Uhispania yaaga Brazil2014
Uhispania iliilaza Australia 3-0
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/uhispania-yaaga-brazil2014.html
Mabingwa watetezi wa kombe la
dunia Uhispania waliepuka fedheha ya kukamilisha mechi za makundi za
mchuano wa Brazil 2014 katika nafasi ya mwisho kwa kuilaza Australia
mjini Curitibia.
Mabao ya Uhispania yalifungwa na David Villa, Fernando Torres na Juan Mata.Mata alifunga la tatu kutoka kwenye pasi ya mchezaji aliyekuwa wa ziada Cesc Fabregas.
Vijana wa Vicente del Bosque sasa wamemaliza katika nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu baada ya kushindwa mara mbili na kushinda mechi moja.
Haya ndiyo matokeo yao mabay zaidi tangu mwaka wa 1991.
