TFF CHINI YA RAIS MALINZI YATINGA BUNGENI NA MIKAKATI YAKE
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tff-chini-ya-rais-malinzi-yatinga.html
Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ukiongozwa na Jamal Malinzi jana (Juni 21 mwaka huu) mjini Dodoma umekutana na
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake
Mheshimiwa Said Mtanda (Mbunge wa Mchunga).
Katika kikao hicho TFF ilielezea mikakati yake ya maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na maandalizi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Msumbiji.
TFF iliiahidi Kamati ya Bunge kuwa itaendelea kuwa inafanya
shughuli zake kwa karibu na Serikali na kamati hiyo ya Bunge.
Katika kikao hicho, ujumbe wa benki ya CRDB ukiongozwa na Meneja
wa Electronic Banking, Bw. Mangire Kibanda ulihudhuria ili kutoa ufafanuzi juu
ya mradi wa kuuza tiketi za elektroniki, mradi ambao maandalizi yanaendelea
vizuri.