TANGULIA TYSON, HAUTASAHAULIKA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/tangulia-tyson-hautasahaulika.html
FILAMU
ya Girlfriend iliyotengenezwa mwaka 2003, ambayo wadau wote
wanakubaliana kwamba ndiyo iliyolipua moto wa watengeneza sinema wa
Kitanzania, inabaki kuwa ndiyo filamu iliyomuweka rasmi George Otieno
Okumu ‘Tyson’ kwenye ramani ya filamu za Kibongo na kumpa heshima kubwa.
George Tyson, Mkenya aliyekuwa akifanya
shughuli zake hapa nchini alifariki dunia wiki iliyopita kwa ajali ya
gari iliyotokea Morogoro alipokuwa akirejea Dar akitokea Dodoma.
Msiba huu mkubwa, umesikitisha wengi,
hasa wadau wa filamu wanaporejea historia ya chachu ya filamu za
Kibongo. Ni jambo lisilopingika kwamba Tyson alitusaidia kujenga
misingi ya ajira kupitia filamu kutokana na mchango wake mkubwa.
Tangu mwaka tuliotengeneza filamu ile,
2003 hadi Tyson alipofariki dunia ni miaka 11 imepita. Matunda yake
yangali yanaendelea kwa sababu moto ule uliowashwa, haujawahi kuzimika
hadi leo, hamasa zilivyowajaa watengeneza filamu zingali zinaendelea na
sasa tasnia hii imepanuka na imesaidia kutoa ajira kwa wengi.
Nafikiri ni wakati muafaka sasa wa mimi
kuandika machache kuhusu filamu ile, nikikazia mchango kwa mtengeneza
filamu marehemu George Tyson na kueleza mengine ambayo ni muhimu sana
leo yakajulikana ili kuweka kumbukumbu juu ya filamu hii ya kihistoria.
Wazo la filamu ya Girlfriend lilikuwa ni
la kwangu na lilitokana na makala yangu mwenyewe ambayo ilichapishwa
kwenye gazeti tumbo moja na hili la Amani (nilikuwa mhariri kiongozi wa
gazeti hilo kipindi hicho) iliyokuwa na kichwa cha habari kilichosema:
HIVI WASANII WA RUNINGA HAWANA WIVU AU UBUNIFU WA MAENDELEO YAO? Ilichapishwa kwenye toleo namba 216 la Novemba 14-20, 2002.
Kwa ufupi makala yenyewe ilihusu namna
ambavyo sinema za Kinigeria zilivyokuwa zinapitishwa kuingia Bongo na
kuuzwa kwa wingi huku wasanii wa nyumbani wakiwa hawaonekani kufanya
juhudi zozote za kuonesha kwamba na wao wanaweza. Wakati ule michezo ya
runinga ndiyo iliyokuwa ikitamba sana.
Niliichukua makala ile kama changamoto
na ndipo nilipoandika hadithi ya filamu ambayo nililenga kuwahusisha
wanamuziki wa Bongo Fleva ambao walikuwa juu kipindi hicho halafu
wachanganyike na wale wa maigizo ya runinga. Lengo la kufanya hivyo
lilikuwa ni kuinua sanaa ya filamu kupitia wasanii wa Bongo Fleva! Wazo
hilo nilishirikiana na mwenzangu, Kessa Mwambeleko.
Lakini mimi sikuwa na ujuzi wowote
kuhusu mambo ya filamu, japo nilikuwa ni mchambuzi wa maigizo
magazetini, lakini sikuwahi kusoma wala kujua hasa filamu
zinavyotengenezwa ndipo tulipokubaliana kumfuata George Tyson. Wakati
huo alikuwa ameshaacha kazi ITV na alikuwa akiongoza Kikundi cha Nyota
Academia kilichokuwa kikipatikana kwenye jumba la utamaduni wa watu wa
Urusi.
Mwanzoni tulikuwa na mzuka wa
kuhakikisha kazi hiyo inafanyika lakini hatukuwa na fedha! Mimi na
mwenzangu tulijipa moyo kwamba fedha tutazipata tu, la msingi maandalizi
kwa ajili ya filamu hiyo yaanze. Wakati huo hata jina la filamu sikuwa
nalo, nilikuwa na hadithi tu mkononi.
Tulikubaliana na mwenzangu kwamba mimi ndiye nikamvae George Tyson ambaye kwa bahati tayari alikuwa ni rafiki yangu na kumweleza mpango wetu.
Tulikubaliana na mwenzangu kwamba mimi ndiye nikamvae George Tyson ambaye kwa bahati tayari alikuwa ni rafiki yangu na kumweleza mpango wetu.
Siku ya pili nilitoroka kazini, nikaenda
‘Russian Culture Centre’ na kukutana na George Tyson. Alinipokea kwa
bashasha zote, nikamweleza kwa kina tunachotaka kufanya na hapohapo
nikamkabidhi hadithi yenyewe na majina ya wasanii wa Bongo Fleva ambao
tulipanga kuwatumia! Kuna mambo mawili nikamhakikishia.
La kwanza nilimwambia kwamba magazeti
yote ya kampuni tunayofanyia kazi ya Global Publishers yataitangaza
filamu hiyo kwa nguvu zote maana wafanyakazi wenzetu wote walifurahishwa
na wazo letu na walikuwa tayari kusaidiana na sisi kwenye jambo hilo.
Jambo la pili, nilimwambia kwamba
wasanii wote wa Bongo Fleva watakaoshiriki ni lazima warekodi wimbo
ambao utakuwa ukipigwa kwenye vituo vya redio kuwamba ndiyo ‘soundtrack’
ya filamu ile.
Tyson si kwamba alikubali kwa moyo mmoja
kuwa muongozaji wa filamu hiyo, lakini pia alipandwa na mzuka wa ajabu.
Akanipa moyo kwamba filamu hiyo itatengenezwa na wasanii wote
tuliowaandika watapatikana! La muhimu ni kwamba sisi tuingie ‘msituni’
kutafuta pesa za kuanza kuwalipa wasanii ‘advance!’
Hapo ndipo palipokuwa na kasheshe!
Kuanzia hapo, vikao baina yetu na Tyson vikawa ni kila siku, nyumbani kwake Kinondoni-Shamba, Dar na kwenye Mgahawa wa Best Bite Namanga.
Kuanzia hapo, vikao baina yetu na Tyson vikawa ni kila siku, nyumbani kwake Kinondoni-Shamba, Dar na kwenye Mgahawa wa Best Bite Namanga.
Hadi leo mimi na Yvone-Chery (Ngatikwa)
‘Monalisa’ ambaye alikuwa mke wa George Tyson kipindi hicho, tungali
tunabishana kwamba jina la filamu ‘Girfriend’ alilitoa nani kati yangu
mimi na yeye! Ila tunakubaliana kwamba ilikuwa ni usiku mmoja ambapo
nilikula chakula cha usiku nyumbani kwao ndipo jina hilo likapatikana!
Kwa bahati nzuri, wasanii wote wa muziki
tuliowaandika ambao ni King Crazy GK, AY, Jay Mo na TID, wote
walikubali na mara moja walianza mazoezi kwenye ukumbi huohuo wa Russian
Culture! Halafu Monalisa, Nina na wengineo ambao walikuwa wakitamba
kwenye runinga kipindi hicho, nao wakajiunga nasi. Hiyo ilikuwa ni
faraja kubwa kwetu, mimi na mwenzangu ambao tulikuwa tunahaha kutafuta
pesa. Moto tuliouchokoza, ulikuwa unawaka!
George Tyson alikuwa na uwezo mkubwa
sana wa kushawishi, akalazimika kuwapiga ‘Kiswahili’ wasanii wale
waendelee na mazoezi na wasubiri malipo yaliyochelewa kidogo!
Nakumbuka mmoja wa watu ambao
walitusaidia ‘kutulindia’ heshima kwamba ‘pesa zipo’ alikuwa ni marehemu
Mohamed Mpakanjia ‘Meddy’. Yeye tulimfuata na akakubali kuzungumza na
wasanii na kuwatia moyo, yeye alikuja mazoezini kwa niaba ya Kepteni
John Komba ambaye naye aliahidi kusaidia!
Wakati huo wote magazeti ya kampuni yetu na kampuni nyingine yalishaanza kuandika juu ya ujio wa filamu hiyo! Watu wakaanza kutafutana mjini!
Tyson aliendelea kuwa nguzo ya kazi ile, maana alifanikiwa kuwatuliza wasanii wote waendelee na mazoezi bila kujua kilichoendelea nyuma ya pazia.
Mungu si Athumani, kwa bahati nzuri tulipata pesa za malipo ya awali za wasanii kutoka kwa mfadhili mmoja ambaye alikubali kulipa! Hapo tukawa tumepiga hatua kubwa.
Tukawalipa wasanii wote pesa nusu za malipo yao na sasa ratiba ikasoma kwamba filamu itaanza kurekodiwa kwenye Ukumbi wa Club Bilicanas, wiki moja baadaye! Vurugu hizo zote tulizifanya kwa mwezi mmoja na wakati huo wote, mkurugenzi wa kampuni tunayofanyia kazi, Eric Shigongo alikuwa amesafiri Mwanza! Huku nyuma, meneja wetu, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ tulikuwa tumemficha! Kiasi kwamba alikuwa hajui ‘movement’ zetu za kutokatoka ofisini zilihusiana na nini.
Wakati huo wote magazeti ya kampuni yetu na kampuni nyingine yalishaanza kuandika juu ya ujio wa filamu hiyo! Watu wakaanza kutafutana mjini!
Tyson aliendelea kuwa nguzo ya kazi ile, maana alifanikiwa kuwatuliza wasanii wote waendelee na mazoezi bila kujua kilichoendelea nyuma ya pazia.
Mungu si Athumani, kwa bahati nzuri tulipata pesa za malipo ya awali za wasanii kutoka kwa mfadhili mmoja ambaye alikubali kulipa! Hapo tukawa tumepiga hatua kubwa.
Tukawalipa wasanii wote pesa nusu za malipo yao na sasa ratiba ikasoma kwamba filamu itaanza kurekodiwa kwenye Ukumbi wa Club Bilicanas, wiki moja baadaye! Vurugu hizo zote tulizifanya kwa mwezi mmoja na wakati huo wote, mkurugenzi wa kampuni tunayofanyia kazi, Eric Shigongo alikuwa amesafiri Mwanza! Huku nyuma, meneja wetu, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ tulikuwa tumemficha! Kiasi kwamba alikuwa hajui ‘movement’ zetu za kutokatoka ofisini zilihusiana na nini.
Na yeye tukamdanganya kwa kumsimulia
kuhusu ujio wa filamu ya wasanii wa Bongo Fleva na sisi tukijifanya
hatuijui! Akapendezwa sana na wazo hilo na kwenda Russian Culture,
akapiga picha na kuja kupamba kwenye kurasa zake za katikati ambazo ni
maarufu sana kwa burudani! Akawa amechangia kuanza kuitangaza! Siku
chache baadaye, Shigongo akarudi!
Na yeye akasoma habari zilizoandikwa
kwenye magazeti (yakiwemo yake mwenyewe) kuhusu ujio wa filamu ile!
Akaipenda sana ‘aidia’ hiyo! Ila akawa hajui ni ya nani!
Kwa masikio yetu tukamsikia akisifia wazo hilo, mimi na mwenzangu tukatazamana!
Huo ulikuwa ni msala! Kwa jinsi bosi huyo alivyokuwa ‘siriaz’ na kazi, haingewezekana tena kuturuhusu ‘tutoketoke’ kwenda kufuatilia kuhusu filamu ile. Na mbaya zaidi, kesho yake ilikuwa ndiyo siku ya mkesha wa kuanza ‘shooting’ pale Club Bilicanas! Hadi hapo, hela ya kulipia ukumbi siku hiyo na gharama nyingine zote tulikuwa bado hatujapata!
Huo ulikuwa ni msala! Kwa jinsi bosi huyo alivyokuwa ‘siriaz’ na kazi, haingewezekana tena kuturuhusu ‘tutoketoke’ kwenda kufuatilia kuhusu filamu ile. Na mbaya zaidi, kesho yake ilikuwa ndiyo siku ya mkesha wa kuanza ‘shooting’ pale Club Bilicanas! Hadi hapo, hela ya kulipia ukumbi siku hiyo na gharama nyingine zote tulikuwa bado hatujapata!
Huku vichwa vikituuma tukakope wapi hela
shooting ianze, huku bosi karudi. Hata kama tukijificha na kwenda
ku-shoot, tayari atajua na akijua pengine filamu ingeishia hapo! Ndipo
mimi na mwenzangu tukakaa kikao na kukubaliana kwamba tumwone meneja
Abby Cool, tumtake ushauri! Kweli tukamfuata, akafurahishwa sana
kugundua kwamba kumbe tulioanza kutikisa mji ni sisi wawili na wa tatu
akiwa George Tyson. Akatushauri tumvae bosi tumweleze ukweli!
Katika tukio la kihistoria kabisa,
Shigongo akalipokea wazo lile na tukamwomba tushirikiane naye
kuitengeneza filamu hiyo! Amini usiamini papohapo baada ya kikao tu,
Shigongo aliidhinisha kwa mhasibu tukachukue shilingi laki saba za
kuanzia kazi Club Bilicanas kesho yake! Ilikuwa ni jambo la kusisimua
sana!
Si tu alitoa pesa, Shigongo alihudhuria shooting yetu ya Bilicanas! Tulipata moyo sana!
Na hapa nataka niseme kitu ambacho watu
wengi hawakuwa wakijua, filamu ya Girlfriend iligharamiwa kwa asilimia
kubwa na Shigongo hadi ilipokamilika na kuzinduliwa kwa kishindo kikubwa
ambacho haijapata kutokea kwa filamu yoyote nchini. Gharama nyingine
ndogondogo kama mazoezi ya wasanii na malipo ya awali tulikopakopa kwa
marafiki zetu! Kiasi tukawa tunanuka madeni!
Mimi na mwenzangu tulifanya juhudi kubwa
kuwasiliana na Prodyuza wa Bongo Records, Paul Mathhyasse ‘P. Funk’
kufanikisha mpango wa kurekodi wimbo uliobeba filamu yenyewe. Japo
tulipanga warekodi wasanii wote, lakini TID na Jay-Mo waliwahi kurekodi
wimbo huo. Wasanii wenzao, King Crazy GK na AY walikuwa waungwana sana,
waliridhika na wimbo ingawa hawakushiriki. Na hiyo ni kwa sababu ulikuwa
ni wimbo mzuri sana.
Girfriend ilizinduliwa mara mbili jijini
Dar, mara ya kwanza ni katika Hoteli ya Golden Tulip, Masaki ambapo
hoteli ilifurika kupindukia kiasi kwamba kuanzia siku hiyo hoteli hiyo
wakagoma kuruhusu uzinduzi wowote mwingine! Na mara ya pili yaani wiki
moja baadaye filamu ilizinduliwa Diamond Jubilee na kujaza watu
vilevile!
Kimsingi, Girlfriend isingefanikiwa
kutengenezwa bila ya nguvu kazi, ujuzi na bidii kubwa sana iliyofanywa
na marehemu George Tyson. Jinsi alivyonipa moyo mara ya kwanza
nilipomfuata kisha yeye kuacha kazi zake zote na kushughulikia filamu
hii, kilikuwa ni kitu cha kuvutia sana. Dairekta mwingine asingekubali
kupoteza muda wake kufanya kazi ambayo hajui angelipwa vipi!
Mei 27, mwaka huu, nilimpigia simu ya
kawaida George Tyson na kuongea mambo yetu ya kirafiki, jambo la ajabu
ambalo lilinishangaza sana ni kwamba George Tyson alicheka sana kwenye
simu siku hiyo. Kichekesho nilichomsimulia kilikuwa kidogo sana
kulinganisha na kicheko alichotoa, alicheka mfululizo kiasi
akaniambukiza na mimi nikacheka kama yeye.
Siku tatu baadaye nikapigiwa simu kwamba rafiki yako, George Tyson amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Tangulia kaka, mchango wako hautasahaulika.
Tangulia kaka, mchango wako hautasahaulika.
Sultan Tamba ni mdau mkubwa wa burudani ambaye alifanya kazi kwa karibu na marehemu George Tyson.
ANGALIA GLOBAL TV ONLINE MUDA WOTE KWA

