TALEBAN LAWAKATA VIDOLE WALIOPIGA KURA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/taleban-lawakata-vidole-waliopiga-kura.html
Maafisa
nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi
mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kaskazini mwa taifa hilo kukanyaga
bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa
urais wa raundi ya pili.Katika tukio jengine kundi la Taleban
limewakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika
uchaguzi nchini humo.
Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.
Raia wa
taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa Waziri wa mambo ya kigeni
Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuwa waziri wa fedha.
Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.

