Flatnews

STRESS FREE LIVE FROM SINTAH JLO BLOG & LIVE UNFILTERED COMMENTS!!

EMMANUEL MBASHA AJITOKEZA (PART 2 YA STORY) Emmanuel Mbasha na mkewe


EMMANUEL MBASHA AJITOKEZA (PART 2 YA STORY)
Emmanuel Mbasha na mkewe


 Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
“Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza,” alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.
“Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea,” alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung’amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
 Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.
Akiwa nje ya kituo cha polisi Jumatatu usiku, binti huyo aliliambia gazeti hili kwamba mara ya kwanza alibakwa mchana Mei 23 na kwamba mtuhumiwa alirudia kitendo hicho Jumapili Mei 25 usiku ndani ya gari katika eneo la Tabata, ambako anadai alifanyiwa kitendo hicho mara mbili.
Hata hivyo, Mbasha alihoji: “Hivi kweli hata kama mimi ni mbakaji, kweli nimbake mtoto wa kumlea mwenyewe mara tatu, yaani Ijumaa halafu nirudie tena Jumapili? Hata kama ni kusingiziwa basi tuhuma hizi zimezidi.”
“Huyu binti nimekaa naye miaka mingi na sijawahi kumfanyia hivyo. Hapo nyumbani kwangu wamekaa mabinti wengi, wakiwamo shemeji zangu wadogo zake na Flora na sikuwahi hata kuwagusa, leo hii kwa nini wananifanyia hivi?”

we do the seeking n you do the judging.......

  1. Wote wa zinzi tu. Cyo mme wala mke. Tofauti ni kwamba mke yuko smart. M bungee wangu anakula adi kesho akamfungulia na Ile studio na kwenye uzinduzi akawa mgeni rasmi. Na nnamjua tena anavyojua kutoa mijihela kwe izo harambeee sasa.
    Reply
    Replies
    1. NAOMBA TUDIGEST HII KWANZA
      ALAFU NTARUDI HAPA KUELEZEA
      YAFUATAYO
      1. Kisa cha mbasha “kubaka"
      2. Milioni 10 alizotoa GWAJIMA
      kwenye msiba wa kulola
      3. Mungu akinipa ujasiri nitamtaja
      kabisa mtu aliye nyuma ya pazia ya
      hii sinema..
      Nimeitoa jamiiforums
      Kulola ni mchungaji wa kwanza wa kilokole Tanzania
      Iko hivi wakuu..
      1. Kisa cha mbasha “kubaka"
      (Sitatoa kila detail ili kulinda identity
      yangu)
      Kabla sijaanza kueleza kisa hiki ni
      vizuri niwaeleze kidogo kuhusu
      Intellijensia ya Gwajima jinsi ilivyo...
      pale kanisani kwake wanavitengo
      mbali mbali amabvyo wenyewe
      wanaviita ‘ministries' na katika
      ministry hizo zipo mbili ambazo ni
      muhimu zaidi i) Media ministry ii)
      Security ministry (hii huwa wanaiita
      ‘mashujaa' wa Daudi)...
      Media - Ministry kazi yake ni
      kulitangaza kanisa mitaani na
      kwenye vyombo vya habari, kueneza
      ‘propaganda' ya kanisa na mambo
      mengine yanayofanana na hayo.
      Security Ministry - kazi yao ni
      kumlinda Gwajima.! Kama umewahi
      kufika pale kanisani utakuwa
      umewahi kuwaona huwa wanavaa
      suti nyeusi na miwani nyeusi (kama
      secret service wa marekani).. wale
      jamaa usiwachukulie poa, majamaa
      wale ni wanajeshi na polisi wastaafu
      na wengine bado wapo kazini..
      Sasa huduma hizi mbili zinaunda
      kitu kama “USALAMA WA TAIFA"
      wa kanisa la Gwajima..
      Turudi kwenye topic sasa....
      Ni ukweli ambao ulikuja kubainika
      hivi karibuni kuwa Mr. Mbasha ana
      mahusiano ya kimapenzi na shemeji
      yake (kwa muda mrefu kidogo) na
      habari hii ikamfikia mpaka florah..
      kipindi hiki florah bado anakaa
      hoteli! Suala hili florah aliwaeleza
      watu wachache sana wakaribu na
      likabakia kuwa siri.. lakini sisi
      wengine tikuwa tunalifahamu muda
      mrefu tu!
      Kuna watu wakamshauri florah
      amuhoji mmewake na florah
      akauchukua huo ushauri akaenda
      kumuhoji Mr. Unaambiwa jamaa
      aling'aka balaa na akakataa kata
      kata kuwa hana mahusiano na
      shemejiye! Basi katika majibizano
      mara jamaa akaropoka kuwa mbona
      hata yeye anafahamu kuwa florah
      anamahusiano na Gwa**** lakini
      hasemi chochote! Weeeeee ilikuwa
      balaa maana hicho kilikuwa kijikikao
      fulani hivi na ndugu kadhaa
      walikuwepo basi kila mtu akashikwa
      na bumbuwazi!!! Unaambiwa flaorah
      hakusema chochote akaanza kulia
      akainuka akaondoka!! Na baada ya
      hapo hata simu za mbasha akawa
      hapokei...
      Inasemekana taarifa zikamfikia
      mchungaji wao Gwajima, basi
      Gwajima akamuita ofisini jamaa
      akakataa kwenda! Sasa katika hizo
      purukushani za kuwasuluhisha
      jamaa kuna siku akatishia kuwa
      atavujisha ushahidi wa mahusiano
      ya huyo mchungaji na mkewe
      florah!! Nahisi hapo ndipo
      alipojiroga..
  2. sintah tuwekee picha za red carpet ya diamond
    Reply
  3. sintah usitake kuniambia hujackia ile clip ya simu alokua anaongea na shemu wake ungeiweka hapa kuongezea mamiiy ndo mwenyewe anaombaga samahani kwa kusimanga lol
    Reply
  4. Msukule wa SintahJune 3, 2014 at 8:45 AM
    maisha ya maigizo yana mwisho mnaumbuka siku hata siku chezeya Yesu wewe? walokole wanafiki usipime endeleeni kujishebedua siri inazidi kujulikana ukatangaze injili gereza la ukonga, siwaelewagi wadada amembaka mdogo wako unasema nimemsamehe khaaa ni ujinga au ni nini?
    Reply
    Replies
    1. DEAR MSUKULE :
      Hiyo ishu ya Flora iko hivi. Flora anatembea na Mchungaji Gwaji...., ndie aliemlipia hotel anayoishi sasa, ndie aliemnunulia lile prado, na ndie aliempeleka Flora kusoma Uk.

      Hii ishu imetengenezwa na uyo mchungaji na flora ili kumuondoa mbasha mbali nao mana alianza kuhoji why yeye na mkewe ni group moja kwenye uimbaji ila Gwaji anambeba Flora tu kwenye safari za ndani na nje ya nchi??

      Kwanini hamjiulizi uyo binti anafamilia yake why alipobakwa akachukuliwa fasta na mchungaji Gwaji??? ....juzi msemaji wa kanisa kajitokeza eti kupinga izo tuhuma Why ajitokeze baada ya ili jambo kutokea?? Alikua wapi siku zote?

      Mtoto kapelekwa kwa gwaji ili afundishwe jins ya kuongea mahakamani, NA uyo daktari wa amana aliefanya vipimo kwa nini ni daktari alekaribu na familia ya uyo mchungaji???

      FROLA HUTAFIKA POPOTE CHOZI LA MUMEO IPO SIKU LITAKUHUKUMU!!!!
      Sinta uibanie hii mi ni mtu wa karibu na familia nataka watu wasome waelewe kinasababisha mbasha na flora wakagombana kupelekea hili jambo kutokea.
    2. Flora kweli uyo mdogoako alibakwa kwanini asiende kukaa kwao kwa familia wanayofwatilia kesi?? Kwanini akakae kwa Gwaji.... ambae wewe na yeye waumini tunawatuhumu mna ukaribu usio wa kawaida,??? Kwanini ukubali mchungaji akulipie hotel wakati una kwako na mumeo??
  5. there's no court like your own conscious...
    Reply
  6. Sinta naomba unisaidie hiyo masters ya international relations and diplomacy inapatikana chuo gani Tanzania au hata Afrika Mashariki? plzzzz plzzzz heeeeeeeelp
    Reply
    Replies
    1. chuo cha diplomasia kurasini uvae official
    2. Acha uvivu wa kufikiri Embu Google bwana!!
  7. Mtoto ya sintahJune 3, 2014 at 9:20 AM
    Doh hadi huruma jamani
    Reply
  8. FLORA NA MUMEWE,NA HUYO BINTI WOTE MALAYA TU .SASA HILO JINA LA YESU INAWAUMBUA
    AGE 17 SIO MTOTO UBAKWE MARA TATU??? UMEBAKWA ULIKUWA UNASIKILIZIA UTAMU???
    FLORA NAYE ETI NAMPENDA MUME WANGU ASILIMIA 100 . SASA ULIMSHITAKI WA NINI SIMNGEENDELEA KUFANYA WEWE NA MDOGO WAKO( GRUP SEX) LAANA ZA DUNIA HIZI ZINAWAKUMBA ,
    NA WEWE FLORA ACHA KUGAWA NJE UMEIVUNJA NDOA YAKO KWA MIKONO YAKO.KICHEUCHEFU KITUPU
    Reply
  9. Gwajima na Flora wanauhusiano. Na ndio chanzo cha ugomvi na mumewe. Na ndo wamepanga njama ya kumflash mbasha ili wao waendelee kula bata.
    Reply
  10. Sintah tuwekee red carpetya Houston ya Diamondplatnumz
    Reply
  11. Sinta mbona umeleta habari nusunusu??? Leta yote umu watu waisome mpk mwisho ndo wataelewa kumbe no mchezo mchafu Flora ameupanga kisa tamaa za pesa. FLORA UYO MCHUNGAJI ANA MKEWE WEWE UNATUMIKA TU AKIKUCHOKA ATAKUMWAGA ABEBE MWIMBAJI MWINGINE!!! Muheshimu mume wa ujana wako we mwanamke. Shetani Mkubwa we!
    Reply
  12. Maswali tata!! huyo Mbasha kama hajabaka why anajificha?? Binti km kabakwa mwnye miaka 17 hakuna majirani wala hana cm??toka ijumaa,jmosi na jumapili ndo kasema why?? Flora ni jeuri ya pesa au ni jamaa anamtia wazimu hadi kuhama ndani na kuishi hotel?? kweli hii ni movie na watuambie mtunzi ni nani na wanatufundisha nn ikiwa wao ni walokole??
    Reply
  13. Mgogoro katika ndoa ya Mbasha na
    Florah ulianza kushika kasi mwaka
    jana mara baada ya Florah na
    Mumewe kuhamia kuanza kusali
    kanisani kwa GWAJIMA (ufufuo na
    Uzima - kawe) wakitokea kanisa la
    MITO YA BARAKA (kariakoo)!
    Inasemekana kuwa mara baada ya
    kuhamia kanisani hapo kwa mualiko
    wa Gwajima (aliwaombe waje kusali
    kwake), mchungaji Gwajima
    alimfanya florah kama kiongozi wa
    Ibada ya SIFA na KUABUDU katika
    mikutani yake!! Kama ni mfuatiliaji
    wa haya mambo utakumbuka kuwa
    mwaka jana Florah alizunguka
    Tanzania nzima akiwa na Gwajima
    wakifanya mikutano ya Injili!!
    Baada ya Muda kidogo Mchungaji
    Gwajima alimpeleka Florah London
    kwaajili ya masomo kitendo ambacho
    inasemekana kilipingwa sana na
    mumewe Mbasha! Ikumbukwe kuwa
    GWAJIMA haiwezi kupita miezi
    miwili pasipo kwenda UK coz
    amefungua kanisa kule (GLORY OF
    CHRIST - UK)!! So katika kipindi
    ambacho florah alikuwa London
    walikuwa wanaonana mara nyingi
    sana na GWAJIMA...
    Baada ya Florah kurudi Tanzania
    ndipo akaanza hii ziara ya
    kuzunguka mikoani na GWAJIMA..
    inasemekana kuwa katika kipindi
    hiki ndipo mahusiano ya kindoa kati
    ya forah na mumewe yalizorota
    zaidi... baada ya ziara kuisha Florah
    arirudi nyumbani lakini she wasn't
    the same (nisiseme zaidi)! Baada ya
    mikwaruzano ya hapa na pale ndipo
    Florah akaenda kukaa hotelini na
    inasemekana hoteli ilikuwa inalipiwa
    na mchungaji GWAJIMA, ikumbukwe
    kuwa ni swala la kawaida kwa
    Gwajima kuwalipia bills mbalimbali
    viongozi wake wa huduma hapo
    kanisani kwa mfano anamchngaji
    anaitwa MAXMILLIAN MACHUM
    amempangishia nyumba ya ghorofa
    pale ubungo na wachungaji wake
    wote wapatao thelethini
    amewanunulia magari!! Lakini hata
    hivyo hii hatua yake ya kumpangia
    hoteli mke wa mtu ilizua maswali
    mengi sana.....
    Reply
  14. KESI YA KUBAKA
    baada ya mrafaruku kutokea jamaa
    akawa dizaini kama amesitisha
    mahusiano na shemejiye na hapa
    kati alikuwa hakai nyumbni kwa
    florah.. lakini inavyoonekana
    mchungaji alitishwa sana na mkwara
    wa jamaa kuwa atavujisha ushahidi
    wa mahusiano yake na mkewe...
    binafsi nahisi mipango ikaanza
    kusukwa na binti akasetiwa kwa ajili
    ya ‘operation tokomeza'!!
    Juzi juzi hapa kabla ya tukio
    kutokea ndio huyu binti amerudi
    kwa florah akijua wazi kabisa dada
    take hayupo! Na kama ujuavyo
    muonja asali aonji Mara moja, jamaa
    kuona mzigo umerudi basi ikabidi
    wakumbushie enzi!
    Sitaki kumaliza huondo wote lakini
    tujiulize maswali haya!!!
    1. Hivi kubaka ndio inakuwa hivi?
    Ni ijumaa mko nyumbani peke
    mnamaliza kula mchana mnakaa
    sebuleni mnapiga stori ‘mizuka
    inapanda mnaamua kuibanjua amri
    ya sita! Kesho yake jumamosi
    anakuja mgeni mnakuwa wapole tu,
    mnavunga mnaitana shemeji! Alafu
    kesho kesho yake jpili mnatengeneza
    mazingira ili muondoke peke yenu
    wawili! Mnafika mahali fulani
    ubungo mnapaki gari mafichoni
    mnaanza kuibanjua amri ya sita!
    Mnatoka hapo mnaenda kanisani
    mnatabasamu kabisa, ibada ikiisha
    mnatengeneza tena mazingira ili
    muondoke peke yenu! Mnafika
    kisehemu chenu mnapaki tena gari
    mnabanjuka! Halafu eti
    amebakwa???????
    Swali la pili la kilujiuliza!
    Kwanini huyu binti baada ya tukio
    kutokea akawapigia simu bodyguards
    wa Gwajima ambao walienda
    kumchukua na kurudi nae nyumbani
    kwa gwajima??? Alafu eti hawa
    bodyguards ndio wanaanza kuwapa
    taarifa ndugu za florah!! Kwanini
    apige simu kule?? Kwanini
    hakuwapigia simu ndugu zake
    kwanza?????

Post a Comment

emo-but-icon

item