PICHA ZAIDI WACHEZAJI WA CAMEROON WAKIPIGANA UWANJANI ZIKO HAPA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/picha-zaidi-wachezaji-wa-cameroon.html
Hata hivyo hasira za beki huyo mwenye umri wa miaka 30, hazikuishia uwnjani, bali zilizoendelea hadi nje ya uwanja kwa kulumbana na Moukandjo, lakini nahodha na mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto’o aliingia kati na kujitahidi kuzituliza hasira za Ekotto.
Kitendo kingine cha utovu wa nidhamu kilichojitokeza wakati wa mchezo wa jana, ambao ulishuhudia Cameroon wakiambulia kichapo cha pili mfululizo katika michezo ya kundi la kwanza, ni baada ya kiungo wa FC Barcelona Alexandre Dimitri Song Billong, kumpiga kiwiko mgongoni mshambuliaji wa Croatia Mario Mandžukić.
Kwa matokeo ya kufungwa mabao manne kwa sifuri, timu ya taifa ya Cameroon imeondolewa katika kinyang’anyiro cha fainali za kombe la dunia za mwaka huu, licha ya kusaliwa na mchezo mmoja dhidi ya wenyeji Brazil