Papa awapokea Peres na Abbas
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/papa-awapokea-peres-na-abbas.html
Papa Francis amewapokea viongozi wa Israil na Palestina katika Vatikani.
Rais Shimon Peres wa Israil na Mahmoud Abbas wa Palestina walikutana Vatikani kuomba amani Mashariki ya Kati.
Viongozi
hao wawili walikutana na Papa nje ya nyumba yake, kabla ya kusafiri
pamoja naye na kiongozi wa kanisa la Orthodox, Askofu Mkuu Bartholomew,
hadi kwenye sherehe katika bustani ya Vatikani.
Wakitarajiwa
kupandisha mzaituni kama alama ya kudumu ya hamu ya pande zote mbili ya
kupata amani baina ya watu wa Israil na Palestina.
Papa
alisema yeye hataki kuhusika moja-kwa-moja na mazungumzo ya amani,
lakini anatumai viongozi hao wakikutana, huenda ikasaidia kupunguza
uhasama kati yao
