PABLO ARMERO AWAONGOZA COLOMBIA KUSHANGILIA KIMAAJABU, JE, ITAKUWA STAILI KALI KULIKO ZOTE KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/pablo-armero-awaongoza-colombia.html
LICHA ya kukosekana kwa mshambuliaji wao nyota Radamel Falcao, Colombia wameanza
vizuri kombe la dunia baada ya beki wa kulia wa Napoli, Pablo Armero
kuwafungia bao la kuongoza katika dakika ya 5 dhidi ya Ugiriki.
Shuti la Armero halikuwa kali kuliko
tuliyoyaona siku tatu za ufunguzi, lakini staili yake ya kucheza
akishangilia bao lake mbele ya benchi la Colombia ilikuwa nzuri na bora
mpaka sasa, labda ndio inaweza kuwa kali zaidi katika mashindano ya
mwaka huu.
Sukuma: Armero akiwaonesha wachezaji wenzake sehemu ya kwenda kabla ya kuanza kucheza akishangilia bao lake .

Twende kazi: Wachezaji wa Colombia wakijiandaa kuanza kucheza kwa mpangilio wakishangilia bao.

Pamoja: Wachezaji wa Colombia wakishangilia kwa pamoja baada ya bao la Armero lililowafanya wawe mbele katika dakika ya tano.

Mikono juu: Colombia wameanza vizuri katika kundi lao la C baada ya kuifunga Ugiriki
