MTOTO WA R KELLY ATANGAZA KUJIBADILISHA JINSIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mtoto-wa-r-kelly-atangaza-kujibadilisha.html
Mtoto wa miaka 14 wa mwanamuziki mkongwe wa R&B wa nchini
Marekani R Kelly ametangaza kubadilisha jinsia yake kupitia mitandao ya
kijamii.Mtoto huyo aitwaye Jaya alizaliwa mwanamke lakini
akachukua uamuzi mgumu na kuwaambia mashabiki zake kuwa sasa hivi yeye
ni mwanaume akiitwa Jay kwakuwa amebadilisha jinsia yake.Lakini
wakati mama yake Andrea Kelly akimuunga mkono mtoto wake kutokana na
hatua hiyo, baba yake R Kelly bado hajazungumza chochote.
Jaya ambaye sasa anaitwa Jay amesema mama yake alifurahishwa sana kwa
kitendo chake hicho na kusema anampenda mtoto wake vyovyote vile alivyo
ambapo anamshukuru mama yake kwa kukubali yeye kubadili jinsia yake na
kuwa mwanaume.
Ameongeza kuwa anaamini yeye sasa ni mwanaume na anataka upasuaji zaidi na tiba ya kumsaidia kuwa vile alivyotakiwa.
Jay amesema akiwa na umri wa miaka sita alijigundua kuwa anavutiwa sana na wasichana lakini hataki mahusiano kwanza.
