MTOTO ATESWA MIAKA MIWILI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mtoto-ateswa-miaka-miwili.html
Mtoto Merina
Mathayo (15) amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (Moi) Muhimbili
Dar es Salaam, baada ya kuteswa na kujeruhiwa kichwani kwa kipigo maeneo
mbalimbali ya mwili na bosi wake kwa miaka miwili..Merina amelazwa Moi
baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Mwananyamala alipokuwa amelazwa
awali, kutokana na majeraha hayo ambayo yanadaiwa kusababishwa kung'atwa
kwa meno na kupigwa kwa vitu mbalimbali mara kwa mara.Akizungumza kwa
shida Merina alisema amekuwa katika hali ya mateso tangu mwaka 2012,
kwani bosi wake huyo ambaye anamtaja kuwa ni mwanasheria mkazi wa Boko
amekuwa na tabia ya kumpiga na vitu mbalimbali akiwa amemvua nguo.
