Masaa kadhaa baada ya timu ya Ivory Coast kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Colombia
katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya kombe la dunia, mastaa wa timu Yaya na Kolo Toure wamepata habari mbaya zaidi.
Wachezaji hao wanaokipiga katika klabu ya Manchester City ya England,
walipokea taarifa ya kifo cha mdogo wao wa kiume ambaye pia ni
mwanasoka.
Msiba huo mkubwa kwa Yaya Toure pamoja na kaka yake Kolo Toure umetokea
jana jijini Manchester ambapo mdogo wao Oyala Ibrahim Toure alifariki
akiwa hosptali The Christie akipewa matibabu baada ya kuugua saratani.
Ibrahim Toure
Ibrahim Toure amefariki akiwa na umri wa miaka 28 na amewahi kuvitumikia vilabu vya
2002-2003: ASEC Mimosas
2003-2006: Metalurh Donetsk
2006-2007: OGC Nice
2009-2010: Al-Ittihad Aleppo
2010-2013: Misr Lel Makasa
2012: Telephonat Beni Sweif (loan)
2013-2014: Al-Safa’ SC