MALINZI ASIMAMISHA UCHAGUZI SIMBA, KISA KAMATI YA MAADILI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/malinzi-asimamisha-uchaguzi-simba-kisa.html
Uchaguzi wapigwa pini: Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametangaza kusimamisha uchaguzi wa Simba sc
RAIS
wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi, jana
aliwaalika waandishi wa habari akiwaomba wafike leo mchana majira ya saa
6:00 katika ofisi za shirikisho hilo kwa lengo la kutoa ujumbe kwa umma
wa wapenda michezo Tanzania.
Wengi
hawakupata majibu juu ya nini Rais Malinzi anataka kuzungumza na
wanahabari kwasababu si kawaida yake kufanya mikutano na waandishi mara
kwa mara.
Akitokea
Brazil kwenye mkutano wa 64 wa FIFA hivi karibuni, hatimaye mchana wa
leo, Rais Malinzi amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa
mikutano wa shirikisho hilo, uliopo makao makuu katikakati ya jiji la
Dar es salaam na kutangaza kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya
Simba ulioatarajia kufanyika juni 29 mwaka huu hadi hapo itakapounda
kamati ya Maadili itakayokuwa na jukumu la kusikiliza masuala ya maadili
kuelekeza uchaguzi huo.
Rais
Malinzi amesema Simba inatakiwa kukamilisha zoezi hilo la kuunda kamati
ya Maadili hadi kufikia juni 30 mwaka huu ili mchakato wa uchaguzi
uweze kuendelea chini ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, wakili, Dkt.
Damas Daniel Ndumbaro.

Mpiganaji: Rais wa Simba sc, Ismail Aden Rage ataendelea kuiongoza klabu hiyo.
Wengi
walijiuliza kwanini TFF imefikia uamuzi huo, lakini Malinzi alifafanua
kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia kuibuka kwa malalamiko mengi ya
kimaadili, hivyo kamati hiyo itayasikiliza na kufikia maamuzi.
Uchaguzi
wa Simba uliopangwa kufanyika juni 29 mwaka huu uliingia sura mpya
tangu Michael Richard Wambura aliopoenguliwa kugombea nafasi ya Urais.
Suala
hilo lilionekana kugusa watu wengi, lakini alipokata rufani na
kushinda, mengi yakaibuka zaidi na baadhi ya wanachama walipinga
kurudishwa kwake katika uchaguzi wa Simba.
Hata
hivyo, Malinzi amekiri kuwa TFF imepokea malalamiko mengi juu ya
ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo,
hivyo ni muhimu kuundwa kwa kamati ya maadili itakayoshughulikia mambo
hayo.
Wakati
huu ambapo kamati itakuwa ikiundwa, kamati ya utendaji ya Simba iliyopo
madarakani kwasasa, chini ya Rais wake, Ismail Aden Rage itaendelea
kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Jana
Rage wakati anazungumza na mtandao huu alisema anajitahidi kuhakikisha
anaacha mchoro au msingi au hata ghorofa moja ya Hosteti za wachezaji
katika eneo lake la Bunju ili kuepukana na gharama kubwa wanazotumia
kuwaweka wachezaji hotelini wanapofanya kambi.
Rage
aliyasema hayo kufuatia uongozi wake kuanza utekelezaji wa ujenzi wa
uwanja wa kisasa ambapo tayari magereda na malori yalishapelekwa kwajili
ya kazi.
