Flatnews

MAJANGA : BABA WA KAMBO AMUUNGUZA MWANAYE MIKONO KWASABABU YA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI




            Mtoto mmoja wa  miaka nane, mkazi wa Mjimwema Songea mkoani Ruvuma amefanyiwa ukatili wa kutisha na Baba yake wa kambo aitwaye Stan Nyoni kwa kumchoma moto mikono yake yote miwili kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.Jeshi la polisi mkoani Ruvuma bado linamsaka mtuhumiwa wa unyama huo,Stan Nyoni ambaye alitoroka baada ya kufanya unyama huo huku mtoto huyo akiwa amelazawa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Songea.
Tukio hilo la kinyama  limewafanya 
baadhi ya madaktari na manesi wa hospitali hiyo kumwaga machozi kutokana na mtoto Nice kufanyiwa kitendo hicho cha kusikitisha cha kuchomwa moto mikono yake miwili na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake

Post a Comment

emo-but-icon

item