Flatnews

KWELI NDOA NI TAMU, AUNT LULU ALILIA BWANA

MKALI  wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu Amina Ngaluma. ...


MKALI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu Amina Ngaluma.
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.
Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.
Marehemu Amina Ngaluma Enzi za uhai wake.
“We acha tu, aliniahidi kunitafutia mume baada ya kugundua nasumbuliwa na wanaume kila wakati lakini ndiyo hivyo tena Mungu akamchukua kabla hajanitimizia ahadi,” alisema Aunt Lulu.
Amina alifariki mwezi uliopita nchini humo ambapo chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni uvimbe kwenye kichwa.

Post a Comment

emo-but-icon

item