Flatnews

Kesi ya Oscar Pistorius yaanza tena kusikilizwa


Oscar Pistorius akiwasili mahakamani May 20, 2014. (AP Photo/Themba Hadebe)
Oscar Pistorius akiwasili mahakamani May 20, 2014. (AP Photo/Themba Hadebe)
Kesi ya mauaji  inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius itaanza tena kusikilizwa  jumatatu baada ya mwezi mzima wa uchunguzi wa akili kuangalia kama ugonjwa wa wasi wasi unaweza kuwa umesababisha hatua alizochukua usiku aliomuuwa mpenzi wake.
Jaji aliyesimamia kesi yake anatarajiwa kupokea ripoti kutoka kwa watalaam watatu na mtalaam wa saikolojia ambaye alimpima mwanariadha huyo.
Uchunguzi huo wa kiafya uliamrishwa na mahakama  baada ya daktari wa saikolojia kutoa ushahidi kwamba Pistorius alikuwa na ugonjwa wa wasiwasi  ambao unaweza kuwa umechangia katika kuuwawa kwa Reeva Steenkamp alfajiri ya February 14,2013.
Pistorius amedai kwamba alimchukulia Steenkamp kama mwizi aliyeingia ndani kwake alipofyatua risasi kupitia mlango wa bafuni.  Mwendesha mashtaka anadai kwamba Pistorius alimuua mrembo huyo mwenye umri wa miaka 29 baada ya mabishano.

Post a Comment

emo-but-icon

item