Kenya yaelekea wapi?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kenya-yaelekea-wapi.html
Mwishoni mwa miaka ya '60, mshairi Abdilatif Abdulla kutoka pwani ya Kenya aliwahi kuandika shairi akiuliza "Kenya Twendapi?", swali ambalo hadi sasa limesalia bila majibu, hasa kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama.
Mkaazi wa Mpeketoni, Kaunti ya Lamu, Kenya, akibeba bango la kutaka amani baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.
Katika kipindi hiki cha Maoni Mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Khelef
anaongoza mjadala unaomulika uwezekano wa mdahalo wa kisiasa katika
taifa hilo la mashariki ya Afrika, na uwezekano wa mdahalo huo kuokoa
hali isielekee kubaya zaidi.Washiriki wa mjadala huu ni Tom Odhiambo, Koigi Wamwere, Ezekieh Gikambi na Aden Mwachu. Kusikiliza makala nzima, bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
CHANZO NI DW IDHAA YA KISWAHILI
