KATIBU KUU WA ZAMANI WA YANGA SC GEORGE MPONDELA KUZIKWA LEO MAKABURI YA KINONDONI
George Mpondela enzi za uhai wake
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/katibu-kuu-wa-zamani-wa-yanga-sc-george.html
ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga ,
George Johnson Mpondela ‘Castro’ atazikwa leo katika makaburi ya Kinondoni
jijini Dar es salaam.
Mtoto wa Marehemu, Dickson Mpondela amesema kuwa
asubuhi hii kuanzia majira ya saa 2:00 mpaka 3:30 mwili wa marehemu utaagwa
nyumbani kwao kigamboni na baadaye mwili utapelekwa kanisani Muhimbili kwa
ajili ya ndugu, jamaa na marafiki wengine kupata fursa ya kumuaga mpendwa wao.
“Hapa nyumbani hatutachukua muda mrefu kuaga mwili
wa marehemu kwasababu watakaohusika ni majirani tu, baadaye saa 4 tutaanza
safari ya kuelekea pale Muhimbili. Kutakuwa na ibada na baadaye watu wataaga
mpaka saa 8 mchana”. Alisema Dickson.
Dickson amesema saa 8 au saa tisa msafara mzima
utaelekea katika makaburi ya kinondoni tayari kwa kumpumzisha mwanamichezo
Mpondela.
Hata hivyo, mototo huyo wa marehemu amesema
familia yao inapata faraja kutokana na baadhi ya wanamichezo na wanachama wa
Yanga kujitokeza kutoa kutoa pole.
Dickson ameomba watu wajitokezea kwa wingi kumuaga mpenda wao.
George Mpondela
alifariki dunia Juni 15 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
jijini Dar es Salaam.
Mpondela
alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga katika uchaguzi uliofanyika
mwaka 1994 baada ya kumshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu George
Ndaombwa.
Bwana alitoa na bwana ametwaa. Pumzika kwa amani
Mpondela.