JOEL CAMPBELL ATAPEWA NAFASI ASERNAL, WENGER AMETHIBITISHA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/joel-campbell-atapewa-nafasi-asernal.html

Joel Campbell aliisaidia Costa Rica kuibamiza Uruguay siku ya jumamosi.
KOCHA Arsene Wenger yuko tayari kumpa fursa Joel Campbell ya kuichezea Asernal.
Kocha huyo wa Asernal ambaye yupo mjini Porto Alegre kama mtangazaji wa Televisheni ya Ufaransa, jumapili jioni alishuhudia Ufaransa ikichapa Honduras maao 3-0.
Lakini Wenger amethibitisha kuwa amepanga kumrudisha tena katika kikosi cha Asernal nyota huyo wa Cost Rica ambaye alifanya kazi nzuri wakiizamisha Uruguay.
Kocha huyo mnamo mwaka 2011 alimtoa kwa mkopo nyota huyo mwenye miaka 21.
‘Hakika atarudi kwetu wakati wa maandalizi ya msimu," Wenger aliwaambia Sportsmail. "Ameimarika vizuri".
Wenger iliikosa mechi ya Costa Rica
kwasababu alisafiri kwenda Porto Alegre, lakini alipokea ujumbe kutoka
kwa kocha wa zamani wa Chelsea Avram
Grant, ambye yuko na luninga ya Israel akimtaarifu jinsi ambavyo
Campbell alicheza vizuri.
Campbell aliifungia Costa Rica bao moja na kutengeneza nafsi moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uruguay mjin Fortaleza.
Campbell
alisaini mkataba na Asernal miaka mitatu iliyopita, lakini muda mrefu
amecheza kwa mkopo , lakini Wenger anahisi sasa imefika muda muafaka wa
kumrudisha katika timu ya kwanza ya klabu yake.
Mara ya kwanza alipelekwa kwa mkopo
katika klabu ya Lorient nchini Ufaransa, halafu Real Betis nchini
Hispania na kwasasa anaichezea timu ya Ugiriki ya Olympiacos, ambapo
amewavutia Manchester United
katika michuano ya ligi ya mabingwa.
