DIEGO COSTA AZOMEWA NA MASHABIKI WA BRAZIL AKIICHEZEA HISPANIA DHIDI YA UHOLANZI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/diego-costa-azomewa-na-mashabiki-wa.html
Alizomewa : Mshambuliaji, Diego Costa alizomewa na Wabrazil wakati Hispania ilipopambana na Uholanzi.
DIEGO
Costa
amezomewa na mashabiki wa Brazil katika mchezo wake wa kwanza katika
ardhi ya nchini mwake tangu alipochagua kuwachezea wapinzani wa `Samba
Boys` , Hispania, katika mbio za ubingwa wa fainali za kombe la dunia
mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo ambaye yuko mbioni kujiunga na Chelsea alianza katika kikosi cha
kwanza cha Hispania dhidi ya Uholanzi kwenye mchezo wa ufunguzi wa kundi
B, lakini alipokelewa na kelele za kuzomewa kwa kitendo chake cha
kuikimbia nchi yake.
Alipogusa
mpira katika dakika ya tano ya mchezo, nyota huyo aliyeifungua Atletico
mabao 35 alizomewa akiwa amevaa jezi ya Spain kwa mara ya tatu.
Aliichezea Brazil katika mechi mbili,
zote za kirafiki kabla ya yeye mwenyewe kuandika barua FIFA akiomba
kuichezea Hispania ambapo ombi lake lilikubaliwa mwezi octoba mwaka
jana.
Wakati wakijiandaa na mechi ambayo
ilikuwa kama ya marudiano ya fainali ya mwaka 2010 dhidi ya Uholanzi,
Costa alisema aliondoka Brazil kwa mapenzi yake mwenyewe na kujiunga na
Hispania.
"Nimethibitisha Hispania ndio taifa
langu na watu wa Hispania wapo nyuma yangu". Alisema. "Ukosoaji wa
maamuzi yangu hauniathiri".
"Brazil ni washindani wa ubingwa,
lakini wapo katika presha kubwa kutoka kwa mashabiki wao.Watu wanahitaji
kuwaona fainali na hiyo inawapa ugumu zaidi".
Baada ya kuiona Brazil ikipata ushindi
katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia, Costa katika mchezo wa
usiku huu amesababisha penati iliyofungwa na Xabi Alonso na kuwapa
Hispania bao la kuongoza.
Nyota huyo mwenye miaka 35 yuko mbioni
kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu kwa dau la paundi
milioni 32, lakini sasa ana presha na taifa la Hispania linalohitaji
kutetea ubingwa wa kombe la dunia.
UHOLANZI WACHAFUA HALI YA HEWA BRAZIL, WAICHABANGA HISPANIA `MKONO KWA MOJA`...ROBBEN, VAN PERSIE MOTO MKALI!


Ndosi hiyo!: Robin van Persie akifunga goli kwa kupiga kichwa matata na kuisawazishia Uholanzi.

Kosa kubwa la mlinda mlango: Van Persie akimpoka Iker Casillas mpira na kufunga bao la nne.

Haamini: Casillas akitafakari baada ya kufungisha bao la nne, huku wachezaji wa Uholanzi wakishingilia bao hilo la Van Persie
Vikosi na viwango vya wachezaji katika mchezo wa leo kwa mujibu wa Joe Callaghan ambaye yupo mjini Sao Paulo. Alama zilizotumika ni 10.
Kikosi cha Hispania:
Casillas 5, Azpilicueta 6.5, Sergio Ramos 5.5, Pique 5.5, Jordi Alba 7,
Alonso 7.5 (Pedro 63), Xavi 7, Busquets 6, Silva 7.5, Diego Costa 7
(Torres 62), Iniesta 7.
Wachezaji wa Akiba: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Fabregas, Mata, Koke, Cazorla, Reina.
Kikosi cha Uholanzi: Cillessen 7, Janmaat 6, Vlaar 7.5, De Vrij 7, Martins Indi 6.5, Blind 7, de Guzman 6, Sneijder 6, De Jong 6.5, Van Persie 8, Robben 8.
Wachezaji wa akiba: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Mwamuzi: Nicola Rizzoli (Italia)
Mchezaji bora wa mechi: Robin van Persie na Arjen Robben
Mabao yote ya Uholanzi yalikuwa ya ajabu. Yote yalitengenezwa kwa pasi murua kutoka wingi ya kushoto kutokea kwa Daley Blind na pasi zilimaliziwa kwa ufundi tofauti na wachezaji Robin van Persie na Arjen Robben.
Wachezaji wa Akiba: De Gea, Albiol, Javi Martinez, Juanfran, Villa, Fabregas, Mata, Koke, Cazorla, Reina.
Kikosi cha Uholanzi: Cillessen 7, Janmaat 6, Vlaar 7.5, De Vrij 7, Martins Indi 6.5, Blind 7, de Guzman 6, Sneijder 6, De Jong 6.5, Van Persie 8, Robben 8.
Wachezaji wa akiba: Vorm, Verhaegh, Veltman, Kongolo, Kuyt, Clasie, Lens, Fer, Huntelaar, Wijnaldum, Depay, Krul.
Mwamuzi: Nicola Rizzoli (Italia)
Mchezaji bora wa mechi: Robin van Persie na Arjen Robben
Mabao yote ya Uholanzi yalikuwa ya ajabu. Yote yalitengenezwa kwa pasi murua kutoka wingi ya kushoto kutokea kwa Daley Blind na pasi zilimaliziwa kwa ufundi tofauti na wachezaji Robin van Persie na Arjen Robben.
Magoli manne yalitokana na makosa ya
mlinda mlango Iker Casillas. Kuelekea mechi ijayo itakayochezwa wiki
ijayo ambayo Hispania wanahitaji ushindi- kuna hoja kuwa kipa wa
Manchester United, David de Gea anaweza kumbadili mlinda mlango huyo
mkubwa wa Hispania.

Bao la tano: Robben (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tano.

Stefan de Vrij (kushoto) akiifungia Uholanzi bao la tatu.

Hapa anageuzwa: Arjen Robben akimpiga chenga Gerard Pique


Iker Casillas (kulia) alipelekwa sokoni


Fungeni midomo: Diego Costa akiwanyooshea kidole mashabiki wa Salvador ambao walimzomea dakika zote alipokuwa uwanjani.

Costa aliangushwa na Stefan de Vrij na mwamuzi kuamuru mkwaju wa penati

Xabi Alonso alifunga penati hiyo
