Diamond Azidi Kumgalagaza Davido Kwenye Maoni ya BET Awards, Sasa Amzidi Katika Instagram ya BET
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/diamond-azidi-kumgalagaza-davido-kwenye.html
‘Die
hard fans’ wanaweza kufanya lolote kuhakikisha wanampa ushindi msanii
wao katika shindano lolote linalohiotaji ushiriki wao hasa wa kupiga
kura au maoni, kama kinachofanywa hivi sasa na mashabiki wa Diamond
Platnumz katika tuzo za BET.
BET
wanaendelea kuweka majina ya nominees katika page zao za mitandao ya
kijamii ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuwaongezea ushawishi wa kupewa
ushindi wasanii wao. Kama ilivyokuwa jana picha ya Diamond imeendelea
kupata likes na comments nyingi katika Facebook ya BET, mpaka sasa ina
likes 2649 na comments 5471 huku Davido akiwa na likes 1465 na comments
619 tu.
Upande wa Instagram ya BET Awards picha ya Diamond iliyowekwa jana usiku na maelezo haya:
‘Dbl tap this pic if you want #DiamondPlatnumz to win #BestInternationalAct: Africa @ the #BETAwards this yr’,
Hadi
sasa ina likes 3275 na comments 4354 huku picha ya Davido katika
akaunti hiyo ya IG ya BET iliyowekwa siku mbili zilizopita ina likes 518
na comments241 tu.

Cha
kushangaza mashabiki wa Diamond wameamua kutoka nje ya kile
kinachotarajiwa baada ya kuamua ku-comment jina la Diamond katika picha
hiyo ya Davido.