Flatnews

COSTA RICA HAWANA MASIHARA KOMBE LA DUNIA, WAICHAPA ITALIA 1-0 NA KUFUZU HATUA YA 16, ENGLAND SASA `BAI BAI`


Circle of life: Costa Rica celebrate their 1-0 victory over Italy which sends them through to the last 16
Costa Rica wakishangilia ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Italia.

TIMU yaTaifa ya Italia maarufu kama Azzuri imeangukia pua usiku huu katika mchezo wa kombe la dunia kundi D baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Costa Rica.
Costa Rica wamepata ushindi wa pili katika kundi lao kwani mchezo w aufunguzi waliwafunga Uruguay mabao 3-1.
Kwa matokoe hayo, Costa Rica wamefuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 tangu mwaka 1958.
  Bao pekee la Costa Rica limefungwa na Bryan Ruiz katika dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza.
Joy: Costa Rica have booked their place in the knockout rounds with a game to spare
Flying Bryan: Fulham flop Bryan Ruiz celebrates the goal which gave Costa Rica a first-half lead
 Bryan Ruiz akishangilia bao lake katika kipindi cha kwanza.
Head boy: Ruiz connects with the deep cross to steer past a helpless Gianluigi Buffon
 Ruiz akiunganisha kwa kicha mpira wa krosi na kufunga bao lake, huku kipa wa Italia   Gianluigi Buffon akiwa hana la kufanya.
Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vya wachezaji. Alama ni chini ya 10.
Kikosi cha Italia (4-3-3): Buffon 6; Abate 5, Barzagli 5.5, Chiellini 4, Darmian 4.5; Motta 5 (Cassano 45mins 6), Pirlo 6.5, De Rossi 5.5; Candreva 6 (Insigne 56mins 6), Balotelli 4.5, Marchisio 5 (Cerci 69mins 6) .
Kadi ya njano: Balotelli

Kikosi cha COSTA RICA (3-4-3): Navas 7.5; Duarte 7.5, Gonzalez 7, Umana 6.5; Gamboa 7, Borges 7, Tejeda 7 (Cubero 67mins 6.5), Diaz 7; Ruiz 7.5 (Brenes 81mins 6) , Campbell 7.5 (Urena 74mins 6.5), Bolanos 8.
Mfungaji wa Goli: Ruiz 44
Mwamuzi: E Ossis (CHI) 5
Mchezaji bora wa mechi: Christian Bolanos
Kwa matokeo haya England kama tayari wameshatupwa nje ya kombe la dunia, huku Italia na Uruguay watakuwa wanagombania nafasi moja ya kundi D wiki ijayo.

Post a Comment

emo-but-icon

item