Watu 6 wafariki dunia kwa kula samaki Kasa
Takriban watu 6 akiwemo mtoto mmoja wameripotiwa kufa Wilayani Pangani mkoani Tanga kwa kula Samaki aina ya Kasa.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/watu-6-wafariki-dunia-kwa-kula-samaki.html
Takriban watu 6 akiwemo mtoto mmoja wameripotiwa kufa Wilayani Pangani mkoani Tanga kwa kula Samaki aina ya Kasa.
Wakazi wanaoishi katika vijiji vilivyopo
pembeni mwa bahari ya Hindi nchini, wameonywa kuacha kitendo cha
kuwinda na kuua viumbe wa bahari wanaohifadhiwa kisheria aina ya
''kasa'' kwa sababu baadhi yao wana sumu ambayo imesababisha watu sita
kufariki dunia akiwemo mtoto wa miezi sita kwa sababu ya kula nyama
yake.
Afisa mradi wa shirika la hifadhi ya
viumbe vyenye hatari ya kutoweka baharini Bwana Boniveture Mchomvu
amewaambia viongozi wa serikali ngazi ya wilaya ya Pangani kuwa baadhi
ya wavuvi wamekuwa wakiwawinda kasa katika fukwe za bahari ya hindi
ambao wamekuwa wakitaga mayai kisha kurudi baharini hatua ambayo
imesababisha kasa kuwa katika hatari ya kutoweka.
Kwa upande wake mhifadhi wa hifadhi
inayohifadhiwa kisheria na serikali ya samaki aliyepotea miaka 200
iliyopita aina ya Silikanti Bi. Anita Jullius amesema uvuvi haramu
unaofanywa na baadhi ya wavuvi wa ndani na nje ya nchi wa kutumia baruti
na nyavu ndogo katika hifadhi za bahari ya Hindi umesababisha miamba
bahari inayohifadhi Kasa kuvunjwa, hatua ambayo imesababisha viumbe hao
kupungua na kuikosesha mapato serikali.
Kufuatia hatua hiyo Afisa Uvuvi wilayani
Pangani Bwana Chitambo Kauta amesema wavuvi haramu wa kutumia baruti
wanatokea katika wilaya za Bagamoyo, Tanga na eneo la Kigombe ambapo
wanapofanya milipuko huharibu matumbawe ambayo ndio mazalia ya samaki
hivyo wanafanya doria lakini tatizo linalowakabili ni raslimali fedha.